Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, May 1, 2015

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA LAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE

 Mgeni Rasmi katika Sherehe za uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.

 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.

Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akiongea na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.

Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengune pindi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula litakapo anza.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.

 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga.

Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama kiuchumi.

 Mh. Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.

Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.

 Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu amezindua Rasmi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.

Akizungumza katika Sherehe hizo Mh. Subira Mgalu amesema kuwa amefurahishwa na Mashindano hayo kufanyikia wilayani kwake katika kijiji cha Kisanga na kuwasihi wakina mama wengi kuchukua fomu za ushiriki, na kusisitiza kuwa wakina mama wa Kisarawe sio wavivu na kuwataka washiriki ipasavyo ili zawadi na mshindi wa kwanza atokee katika wilaya hiyo. 

Aliongeza kuwa Shindano hilo linampa mwanamke uwezo wa kutambua haki zake hasa za umiliki wa Ardhi na kuongeza kuwa ni shindano ambalo mshiriki anahitaji kuwa mbunifu,mwenyeuzoefu ili waweze kubadilishana mawazo na kuwa na mbinu za kisasa za kilimo bora.

Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona alitambulisha rasmi kuwa kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hilo na kuwa shindano hilo linatarajia kuanza rasmi mwanzoni mwa mwezi wa Nane na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV na zawadi ya Mshindi wa kwanza kuwa Shilingi Milioni Ishirini za Kitanzania ambapo Mshindi atapata kwa njia ya kununuliwa vifaa na zana za Kilimo.

Eluka  alizungumzia historia fupi ya shindano hilo ambalo sasa ni mwaka wa nne kuendeshwa na kusisitiza kuwa lengo kuu ni kumfanya mwanamke atambulike katika jamii kuwa nao wakiwezeshwa katika kilimo wanaweza pia wanaweza kumiliki hata ardhi na kuongeza kuwa shindano hilo linawapa wakina mama njia za kisasa za kuendesha Kilimo.

Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya Fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la  Mama Shujaa wa Chakula.

No comments:

Post a Comment