Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 17, 2015

WANACHAMA CCM WAMIMINIKA KUMDHAMINI DAVIS MOSHA....!


Ikiwa hali ya kisiasa nchini Tanzania inazidi kupamba moto katika Wilaya mbalimbali za Tanzania ikiwa ni siku chache kabla ya kipenga cha kuanza kwa kampeni za vyama vya siasa kuwanadi wagombea wake majukwaani kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa kumi. Hali ya kisiasa ndani ya jimbo la Moshi inazidi kuchukua sura mpya baada ya Mgombea kupitia chama cha Mapinduzi Mh. Davis Elisa Mosha kuchukua fomu ya kuteuliwa kugombea kupitia ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Taifa ngazi ya wilaya.


Wanachama wa ccm wakiingia mmoja mmoja kukamilisha zoezi la udhamini wa Mgombea ubunge kupitia ccm

 Baada ya kuchukua fomu hiyo ambazo zinamlazimu kupata sahihi zisizopungua 30 kutoka kwa wanachama wa wa ccm walio ndani ya Manispaa ya Moshi. Hali imepokelewa kwa hisia tofauti na wanachama baada ya mamia ya wanachama kumiminika ndani ya ofisi za ccm za kata na matawi kwa ajili ya kutaka kumdhamini mgombea huyo wa nafasi ya ubunge kupitia chama cha mapinduzi.

Katibu Msaidizi na Muhasibu Mkuu wa ccm wilaya ya Moshi Mjini Bi. Donatha Mushi akijaza fomu ya udhamini baada ya kuhakiki jina na uwanachama wa Mdhamini ofisi ya chama  leo


Tuliweza kuzungumza na katibu msaidizi wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi 
Bi. Donatha Mushi na alikiri kutokea kwa jambo hilo na akaongeza kuwa chama kimeweka utaratibu wanachama wenye sifa za kumdhamini Mgombea wawasili katika ofisi za Chama za wilaya na kuweza kujisajili kwa ajili ya kumdhamini na baada ya kutoa maelekezo hayo asubuhi ya leo amejikuta akipokea kundi kubwa la wanachama ambao wanataka kumdhamini mgombea huyo na kuzidi idadi inayotakiwa ambayo ni isiyopungua wadhamini ishirini na sita (26) huku kwenye fomu kukiwa na sehemu za wadhamini thelathini tu (30) ambapo ishara hiyo ni kuonesha jinsi gani wanachama wa Moshi na wananchi kwa ujumla wanahitaji mabadiliko ya kweli na kuomba kila kata kupeleka mdhamini mmoja na kwingine wawili ili kuweza kuhakikisha kila kata inapata haki ya kumdhamini mgombea wao.

Kada wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kiboriloni Ndugu Willy akijaza fomu ya Kumdhamini Mh. Davis Mosha

Mwanachama Anthon Kimambo kutoka kata ya kiboriloni alisema amewasili ofisi za Wilaya saa moja asubuhi baada ya kupata maelekezo kutoka katika kata kuwa zoezi hilo linafanyika ndani ya ofisi za wilaya na anashukuru Mungu ameweza kumdhamini Mgombea huyo ambaye ni Mkombozi wa Jimbo la Moshi na alimaliza kwa kumuita Jembe.

Bi. Sia R. Shayo akijaza fomu ya kumdhamini Mh. Davis Mosha


Kwa upande wa Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Ndugu Davis Mosha alipoulizwa juu ya Muamko huo wa wanachama alisema huu ni wakati wa mabadiliko na ni wakati wa kuwaacha wananchi wachague kiongozi wanayetaka kumchagua na ametoa wito wananchi kujitokeza katika mikutano ya wagombea wote pindi filimbi ya kuanza kwa kampeni itakapopulizwa na kusikiliza sera zao na mwishoni watajua ni yupi anaweza kuwaongoza. 
"Tutakutana katika mikutano na nitazungumza nanyi, Mimi si mtu wa maneno ni mtu wa vitendo na nina nia ya dhati kushirikiana na wananchi wa Moshi katika kuijenga Moshi Mjini"
Alimaliza kuongea Ndugu Davis Mosha.

No comments:

Post a Comment