Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, August 15, 2015

DAVIS MOSHA AFUNGUA PAZIA LA UCHUKUAJI FOMU MOSHI MJINI

Nia thabiti ya Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Davis Mosha imeanza Rasmi mapema leo baada ya Mgombea huyo kuchukua Fomu za kuwania Ubunge ndani ya Jimbo la Moshi Mjini.

Uamuzi huo wa kulitaka jimbo hilo unathibitisha kauli zake ambazo amezitoa jana katika mkutano wa waandishi wa habari kuwa ana nia ya dhati ya kulikomboa jimbo la Moshi mjini na atahakikisha anatumia muda vizuri katika kuanza mchakato wa kukamilisha taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kukamilika kwa mchakato wa ndani ya chama wa kumpa ridhaa ya kugombea kupitia chama cha mapinduzi.


Mh. Devis Mosha akiwa na Fomu ya Kugombea ubunge nje ya Ofisi ya Hlmashauri ya manispaa ya Moshi pichani pamoja na mtoto wake Daniella Davis

Akikabidhiwa fomu ya Kugombea nafasi ya hiyo ya Ubunge mbele na Msimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndani ya Jimbo la Moshi ndugu Shabani Mtarambe ndani ya ofisi ya Halmashauri ya manispaa ya Moshi. Mgombea huyo aliongozana na Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Moshi mjini Bi. Elizabeth Minde, Katibu wa ccm Wilaya ya Moshi Mjini ndugu Loth Olemesele, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ccm Taifa kupitia wilaya ya Moshi Mjini na Kamanda wa Vijana wilaya ndugu Agrey Marealle, Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Mjini Ndugu Abdallah Thabit pamoja na Mke wake Mrs Davis Mosha na watoto wake Edger Devis Mosha na Daniella Devis Mosha.


Edger Davis Mosha akiwa kambeba Daniella Devis Mosha wakimsindikiza baba yao kuchukua Fomu


Viongozi wa ccm wakimsindikiza Davis Mosha kuchukua fomu katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Fomu hiyo Ndugu Davis Mosha alisema hakuona haja ya kusubiri zaidi ya kutimiza jukumu ambalo wananchi wa Moshi Mjini wanatarajia kumtuma hivyo basi akaona ni vyema kuwahi tiketi yake mapema ambayo itamuwezesha kugombania nafasi hiyo na tiketi hiyo ni Fomu ya Kugombea nafasi ya Ubunge inayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuahidi kuijaza kwa kufuata maelekezo aliyopata kutoka katika tume hiyo ili kuhakikisha anaingia katika kinyang’anyiro cha ukombozi wa jimbo hilo.


Mh. Davis Mosha akitazama fomu aliyokabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi ndugu Shaban Mtalamba

Hata hivyo Msimamizi wa Uchaguzi ndani ya Jimbo la Moshi mjini alitoa Pongezi kwa mgombea huyo kwa kuongoza kwa kuwa wakwanza kuchukua fomu kati ya wagombea wa vyama mbalimbali walioomba nafasi hiyo. Lakini pia alichukua nafasi hiyo kuwasihi wagombea uunge kuhakikisha wanajaza fomu hizo kwa uangalifu na umakini mkubwa kulngana na maelekezo yaliyotolewa na tume hiyo.


Mgombea Ubunge Mh. Davis Mosha akiwa amepozi na makada wa ccm baada ya kuchukua fomu

No comments:

Post a Comment