LINDI mwanafunzi
wa bweni wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya kata ya Mnero,
tarafa ya Ruponda, wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, Agnes Jeremiah
(18) ameuwawa kwa kunyongwa na watu wasiofahamika usiku kisha mwili wake
kutupwa kichakani.
Habari
za uhakika kutoka wilayani humo na ambazo zimethibitishwa na Jeshi la
Polisi zinaeleza mwanafunzi huyo alinyongwa Februari 27, mwaka huu saa
4:30 usiku.
Mashuhuda wamesema kuwa Agnes alikuwa na tabia kutoroka bwenini nyakati za usiku na kwenda nje ya shule.
“Taarifa
ambazo tunazisikia huyu marehemu alikuwa akitoroka bwenini usiku na
kwenda anakokufahamu mwenyewe kabla ya kurejea alfajiri,” alisema mmoja wa watoa ambaye hakupenda jina lake litajwe
Kamanda
wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga amekiri kutokea kifo cha
mwanafunzi huyo, na kueleza uchunguzi walioufanya umebaini alikuwa ni
tabia ya kutoroka bwenini nyakati za usiku na kwenda kwa mpenzi wake wa
kiume.
“Ni
kweli taarifa ya kifo cha huyo mwanafunzi Agnes Jeremiah ambaye ni
mkazi wa kijiji cha Mandawa, akiwa bwenini huko Mnero Sekondari
alitoroka usiku kwenda kwa mwanaume,” alisema Mzinga.
Mzinga
alisema uchunguzi unaonyesha mwanafunzi huyo alipofika eneo la kichaka
kilichopo karibu na kanisa la Roma, alibakwa na wanaume kisha kunyongwa
shingo na mwili wake kutelekezwa papo hapo.
Akasema
katika kufuatilia tukio hilo, wanamshikilia mkazi wa kijiji cha Mnero
Ngongo, Abdallah Ismaili (19) ambaye ni dereva wa bodaboda kwa mahojiano
zaidi.
”Inasemekana
huyu dereva wa bodaboda ndiye aliyekuwa akienda Shuleni hapo kumchukuwa
na kumpeleka kwa mwanaume wake ambaye kwa sasa ametoweka kijijini
hapo,” alisema Mzinga.
Hata
hivyo, kamanda huyo wa Polisi Lindi hakuwa tayari kutaja jina la
mwanaume anayedaiwa kuwa na mahusiano na mwanafunzi huyo, kwa maelezo
kwamba anaweza kuvuruga upelelezi.
“Tunaendelea
kumsaka huyu mwanaume wake aliyekuwa akipelekwa mwanafunzi huyu, hivyo
iwapo tutamtaja jina tunaweza kuharibu upelelezi wetu.”
Source: Africaswahilimedia
No comments:
Post a Comment