Mchezo wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati ya Manchester United na Leicester City  umeifanya Man United izidi kujiwekea hitoria nzuri ya kutwaa taji hilo baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa 1.

Furaha ya Manchester United ambayo iliwekwa na Jesse Lingard na Zlatan Ibrahimovic imeifanya Manchester United kuwa timu yenye mafanikio makubwa zaidi katika kushinda kikombe hicho kwa kufikisha vikombe ishirini na moja (21) rekodi ambayo haijafikiwa na vilabu vingine, Liverpool ikishika nafasi ya pili na vikombe kumi na tanio (15), Arsenal ikishikilia nafasi ya tatu na vikombe kumi na nne (14).

Hata hivyo pamoja na kuibuka na ushindi huo, kocha wa Man United, Jose Mourinho amesema ushindi wa mchezo wa ngao ya jamii na kutwaa ubingwa anautoa kwa aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Louis Van Gaal kwani ndiye aliyewawezesha kupata nafasi ya kucheza mchezo huo.

Ushindi huu ninautoa kwa Mr. Van Gaal na kwa wachezaji saba ambao niliacha kuwapanga katika mchezo wa Leicester, Van Gaal ndiye ambaye ametufanya kupata nafasi ya kucheza huu mchezo bila yeye tusingepata hii nafasi namshukuru sana kwa hilo, "Kwa wachezaji niliowaacha haikuwa na jinsi ni lazima nifanye maamuzi lakini bila kuwa Depay, Jones, na Ashley Young katika benchi sio jambo rahisi lakini ilibidi kufanya hivyo na huu ushindi ninautoa kwao,” alisema Mourinho.