Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru, Mlima Kilimanjaro baada
ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza
kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka.
Gaudence Lekule akipanda mlima Kilimanjaro huku akikimbia wakati akiweka
rekodi baada ya kutumia muda wa saa 8:36 mapema mwaka huu.
Lekule akifurahia mara baada ya kufanikiwa kuweka rekodi ya kutumia muda wa saa 8:36 kupanda Mlima Kilimajaro na kushuka.
MTANZANIA, Gaudence Lekule (31) anayeshiriki michezo ya kupanda milima
kwa kasi (Mountain Run) amemuomba Waziri mpya wa Habari,Utamaduni Sanaa na
Michezo ,Dkt Harison Mwakyembe kutupia jicho michezo mingine kwani ina nafasi
kubwa ya kutangaza na kuletea sifa taifa.
Lekule anayeshikilia rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza Duniani kupanda
kwa muda mfupi katika Mlima Kilimanjaro akitumia muda wa jumla wa saa 8:36
alitoa wito pia kwa kampuni,taasisi binafsi na za serikali kujitokeza kudhamini
wanamichezo kutokana na eneo hilo upo uwezekano wa kujitangaza zaidi kidunia.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum,Gaudence alisema kwa
sasa yupo katika maandalizi ya kuweka rekodi mpya katika milima mirefu na
maarufu Duniani kwa kufanya mazoezi ya awali hapa nchini na baadae nje ya
nchi.
“Nashukuru kuitangaza Tanzania kidunia na tayari nimepata mialiko
mingi ya kwenda nje kushiriki mashindano ya Mountain Run ,Lengo langu ni
kuweka rekodi katika milima mirefu duniani hivyo bado naendelea na mazoezi na
nitaendelea kufanya mazoezi hapa kwetu na badaae nje ya Tanzania”alisema
Gaudence.
Alisema hadi sasa rekodi ya Dunia inashikiliwa na raia wa nchi ya
Ecuador, Karl Egloff aliyetumia muda wa saa 6:53 kupanda na kushuka Mlima
Kilimanjaro ,rekodi aliyoweka mwaka 2014 akivunja rekodi ya Kilians
Jornet raia wa Hispania aliyetumia muda wa saa 7:20 kupanda na kushuka
mlima Kilimanjaro mwaka 2010.
Lekule alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni mabadiliko hali ya hewa
inayochangia kushindwa kufanya mazoezi na upatikanaji wa mahitaji kama chakula
pamoja na mavazi kwa ajili ya mchezo huo unafanyika kuanzia urefu wa mita 3500
hadi 5800.
Akizungumzia kilichomsukuma kushiriki mcezo mchezo huo,Lekule ,mkazi wa
kiraracha Marangu wilaya ya Moshi alisema raia wa kigeni wamekuwa wakishiriki
katika michezo ya aina hiyo kwa ajili ya kuweka rekodi hivyo akaona ni wakati
wa waafrika pia kushiriki katika uwekaji wa rekodi Duniani.
Alisema raia wa Ecuador ,anayeshikilia rekodi ya dunia aliposikia
ameweka rekodi akiwa ni mwafrika na Mtanzania wa Kwanza alituma salamu za
pongezi huku akimtaka kwenda kwenye milima iliyopo nchi za nje kutafuta rekodi
nyinine.
“Egloff alifurahi sana na kunipa moyo na kunitaka nikatafute
rekodi nje ya Afrika kwa sababu nina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri Ulaya
na kuipa sifa Tanzania,ni ngumu sana mtu kukimbia kwenye urefu kama uliopo
Mlima Kilimanjaro na katika maisha inahitaji moyo sana.”alisema Lekule.
Rekodi za kidunia.
Mara ya kwanza rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kasi kwa
Afrika ilikua inashikiliwa na Saimon Mtui akitumia muda wa saa 9 : 20 mwaka
2006, baadae raia wa Hspania Kilians Jornet alitumia muda
wa saa 7:20 mwaka 2010.
Mwaka 2014 ndipo Karl Egloff raia wa Ecuador anayeshikilia
rekodi ya Dunia hadi sasa alitumia muda wa saa 6 :53 mwaka 2014
na sasa Mtanzania Gaudence Lekule ameweka rekodi ya kuwa
Muafrika na Mtanzania wa Kwanza akitumia muda wa saa 8:36.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment