BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda
  Baba wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda akilia na kufarijiwa
  Usu Mallya akilia baada ya kushuhudia mzee Steven Mwaitenda akibubujikwa na machozi mbele yao
  Mkurugenzi
 Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (kushoto) akiwa na Mkuu wa 
Kitengo cha 
Habari na Mawasiliano, Lilian Liundi walipomtembelea Dk.  Ulimboka 
kumfariji jana
  Mzazi akimlilia mwanaye Dk. Ulimboka kwa uchungu MOI
  Baadhi ya wanaharakati anuai wakiwa na maua walipomtembelea 
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka kumfariji jana
  Baadhi ya wanaharakati wakiwa na nyoso za hudhuni baada ya kilio cha baba wa Dk. Ulimboka jana
 BABA
 wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda amejikuta 
akiangua kilio kwa uchungu mbele ya wanaharakati ambao walimtembelea 
mwanae, Dk. Steven Ulimboka kumpa pole kufuatia tukio la kutekwa na 
kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.
 Hali
 hiyo ilitokea jana jioni katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili 
(MOI), ambapo wanaharakati kutoka taasisi na asasi mbalimbali za utetezi
 wa haki za binadamu walifika kwa lengo la kumpa pole Dk. Ulimboka 
kufuatia kitendo kilichomfika.
 Mzee
 Mwaitenda alijikuta akibubujikwa na machozi na kushindwa kuendelea 
kuzungumza alipokuwa akitoa shukrani kwa wanaharakati hao, kwa niaba ya 
mwanaye ambaye wanaharakati hao walishindwa kumuona wote kutokana na 
hali yake ilivyo sasa.
 “Niseme
 wazi nimefarijika sana kwa ujio wenu kumwona mwanangu dhidi ya mambo ya
 kikatili aliyofanyiwa akitetea haki za wengine…,” alisema mzee 
Mwaitenda kabla ya kushindwa kuendelea na kuangua kilio mbele ya 
wanaharakati.
 Baada
 ya tukio hilo baadhi ya wanaharakati walimshika wakishirikiana na 
wanafamilia ya mzee Mwaitenda na kumbebeleza kisha kumtoa mbele ya 
mkusanyiko huo wa wanaharakati na kumrudisha wodini huku wakimfariji.
 Wakizungumza
 mara baada ya tukio hilo wanaharakati wameelezea kusikitishwa na 
vitendo vinavyoendelea MOI eneo ambalo amelazwa kiongozi huyo wa 
madaktari ambavyo vimeendelea kutishia usalama wa Dk. Ulimboka.
 Akifafanua
 zaidi mwakilishi wa wanaharakati hao, Markos Albania alisema taarifa 
walizozipata usiku wa juzi kuna wagonjwa ‘feki’ ambao walijitokeza MOI 
huku wakitaka kulazwa wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) alipolazwa Dk. 
Ulimboka lakini baadaye waligoma kuingizwa wodini.
 “Wapo
 wagonjwa ambao waliletwa na kutaka kupelekwa ICU moja kwa moja…kuna 
watu wanakuja usiku wa manane wakitaka kumtembelea Dk. Ulimboka…matendo 
yanayoendelea kutokea ukilinganisha na kauli za Serikali zilizotolewa 
bungeni yanatishia usalama na uhai wa mgonjwa,” alisema Albania.
 Aidha
 amesema kitendo cha vyombo vya usalama kuendelea kumuhoji Dk. Ulimboka 
akiwa hoi hospitalini si vya kiungwana kwani tayari muhusika amewataja 
hadi kwa majina watu ambao anawashuku lakini hadi sasa hakuna 
aliyechukuliwa hatua yoyote.
 Pamoja
 na hayo wanaharakati hao wameitaka Serikali kuunda tume huru 
mchanganyiko na raia ambayo itachunguza kiundani suala hilo, kwani 
hawana imani na Jeshi la Polisi ambalo limedai kuunda timu ambayo 
inachunguza kwa kina suala hilo.
 Dk.
 Ulimboka ambaye ni kiongozi wa madaktari ambao wanaendelea na mgomo wan
 chi nzima kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao alitekwa juzi na 
watu wasiojulikana na kupigwa na kuteswa kikatili kabla ya kutelekezwa 
katika msitu wa Mabwepande.
 
 
 
No comments:
Post a Comment