Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 29, 2012

WAZIRI WA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO,MH.DKT. FENELLA MUKANGARA AMEPATA AJALI MBAYA....!

 Mh.Dkt. Fenella Mukangara

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh.Dkt. Fenella Mukangara amepata ajali mbaya mchana Tabora mchana wa leo tarehe 29/6/2012ajali hiyo imetokea maeneo ya  Nzega Mkoani Tabora wakati akiwa njiani kuelekea Jijini Mwanza kwenye Ufungunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo Vishale (Darts) yanazinduliwa leo Jijini humo.

Mh. Mukangara anasema chanzo chake ni kuchomekewa na basi moja la abiria (ambalo hakulitaja jina lake).

Hapa namnukuu "Ni kweli tumepata ajali hapa maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati tukiwa njiani kuelekea jijini Mwanza ambako leo kunafanyika ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Darts, tunashukuru Mungu wote tumetoka salama japo tumepata majeraka katika sehemu mbali mbali za mwili."mwisho wa kunukuu.Tunaendelea kuwasiliana na Mh. Mukangara na tutaendelea kupeana taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment