 
  
 
Hali
  ya afya ya Dkt. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha  
Madaktari Tanzania, inaendelea vyema baada ya kushambuliwa na watu  
wasiofahamika usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam.
Dkt.
  Ulimboka aliokotwa jana akiwa hajiwezi na mwili ukiwa na majeraha 
mengi  baada ya kupigwa na watu hao na baade kufikishwa Hospitali ya 
taifa  Muhimbili na wasamaria wema. 
Ulimboka
  anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhumbili kitengo
  cha mifupa MOI aliko lazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)  
huku jopo la madaktari Bingwa wakiendelea kumnusuru.
 
 
 
No comments:
Post a Comment