Pichani juu ni chereko chereko katika harusi ya Hassan Musa ‘Super Nyamwela’ na Hawa Maulid.
Na Gladness MallyaMWANAMUZIKI wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’, Hassan Musa ‘Super Nyamwela’ amevunja ukimya na kuamua kubeba jumla msichana alimpachika mimba aitwaye Hawa Maulid, Ijumaa lina mchongo kamili.
Super Nyamwela alifunga ndoa Jumapili iliyopita kwenye Msikiti wa Kinondoni-Studio, Dar es Salaam na kufuatiwa na sherehe ‘hevi’ iliyofanyika nyumbani kwa Hawa maeneo hayo ya Kinondoni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wenzake.
Baada ya ndoa na tafrija hiyo iliyoshuhudiwa na mwandishi wetu, jioni ya siku hiyo pati nyingine ya kukata na shoka iliendelea kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar ambapo wageni waalikwa walipata nafasi ya kuserebuka huku wakila na kunywa na kuwatuza maharusi.
Akizungumza kwa furaha, Super Nyamwela alisema anamshukuru Mungu kwa kumpatia mke mwema kwa mara nyingine baada ya kukaa muda mrefu kutokana na mke wa kwanza kufariki na kumuachia watoto wawili.
No comments:
Post a Comment