NBA superstar Tony Parker ambae alijeruhiwa kwenye ugomvi kati ya mwimbaji Chris Brown na rapper Drake amefungua mashtaka dhidi ya club ya usiku palipotokea ugomvi huo huko New York Marekani akidai kulipwa fidia ya dola milioni 20, ambapo dai lake kubwa ni club hiyo kuwaruhusu mahasimu Drake na Chris Brown kuwepo ndani ya club hiyo kwa wakati mmoja.
Staa huyo wa San Antonio Spurs alifungua kesi hiyo kwenye mahakama ya jimbo la New York alhamisi na ameishutumu club hiyo kwa uzembe kwenye ishu za ulinzi.
Parker aliumizwa na vipande vya chupa vilivyomrukia jichoni ambapo pamoja na kuyazungumza hayo bado mpaka sasa mmiliki wa club hiyo ameiambia TMZ hajapata taarifa rasmi za kushtakiwa.
No comments:
Post a Comment