MTOTO mchanga aliyezaliwa muda mfupi na kutupwa chooni katika eneo la
Hosteli ya Lilian Ngoyi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)
cha Morogoro, anadaiwa kufanyiwa hivyo na mwanafunzi wa kike anayesoma
hapo.
Tukio hilo la kuhuzunisha, lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya saa nne
asubuhi kwenye chemba (mifereji ya maji machafu) za hosteli hiyo ambazo
zilikuwa zimekwamba kwa kufurika maji baada ya kichanga hicho kushindwa
kupenya kwenye shimo la chemba mojawapo.
Mmoja wa wahudumu wa usafi chuoni hapo, Andrew Seluhimbo, ndiye
aliyegundua tukio hilo la kuhuzunisha baada ya kugundua kwamba
kilichokuwa kimesababisha kuziba kwa mifereji hiyo ni mwili wa mtoto mfu
wa kiume.
Hii ni mara ya tatu kwa miili ya vichanga kutupwa katika Manispaa ya
Morogoro katika kipindi cha siku nne ambapo mwanzoni ilitokea katika Mto
Morogoro eneo la Mji Mpya, ikafuatia huko Kihonda Mizani kabla ya hili
la eneo la SUA.
No comments:
Post a Comment