MTAZAMO WA MACTEMBA KUHUSU SAKATA LA DOGO JANJA!!!
MTAZAMO WA MACTEMBA KUHUSU SAKATA LA DOGO JANJA!!!
Mactemba
binafsi namfahamu tangu kitambo kama mmoja kati ya wapenzi na mdau
kubwa wa muziki wetu wa kizazi kipya,jana nilipita katika ukuta wake wa
facebook nikaona kaandika ujumbe huu kama "MTAZAMO" wake kutokana na
sakata linalovuma sana kwa sasa la kuvunjika kwa uhusiano wa msanii huyo
Dogo Janja na meneja wake MADEE wa kundi la Tip Top connection!
namnukuu:
"Nimefuatilia
kwa karibu suala la Dogo Janja na Madee kwangu mimi si jambo jipya
maana hiyo ni hali ambayo hata Fella anaitumia kwa Dogo Aslay na
mtayasikia pia siku si nyingi, na sio hao watoto tu kuna wasanii wakubwa
sana wanaimbishwa show bure ama kulipwa laki 1 na hao wanaoitwa
waendeleza vipaji... Tip top, Wanaume Tmk ya Fella na makundi mengi ni
ya kinyonyaji sana ila watu wanakosa pa kupaza sauti...
Nyuma ya wizi huu kuna mtandao mkubwa ambao ViNEGA wa Anti Virus
tumekuwa tukiongea na kuwaambia wasanii kuamka ili kupata ukombozi wa
kweli katika sanaa... Hebu ona msanii kama Mr Blue na sifa zote miaka ya
nyuma mpaka akaishia form 1 muulize leo ana mafanikio gani zaidi ya pea
za jeans na supra??? Hao wanaopigiwa debe wamefanikiwa ndio hao wakina
madee wanaowaibia wazi wakina Dogo Janja na kuwafanyia unyanyasaji wa
kijinga... Mtandao wa wizi na dhuluma kwa wasanii ni mkubwa na ni nadra
kupata wasanii wenye mafanikio ya kweli kama Lady Jaydee ama Ay maana
wengi wa wasanii ni wajinga na wapuuzi wakiamini wakipinga kuibiwa
watabaniwa promo na hao wezi so wanaendelea kufanya show za laki moja na
kuishia kununua jeans feki na supra feki na kukaa maghetoni maana
hawawezi kuafford kupanga makazi yenye hadhi... Amkeni wasanii wa
Tanzania" amemaliza!!!!
No comments:
Post a Comment