Asha Rose Migiro
ALIYEKUWA
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Asha-Rose Migiro anatarajia
kurejea nchini leo baada ya kumaliza kazi zake katika Umoja huo na
amewashukuru Rais Jakaya Kikwete na Watanzania wenzake kwa jinsi
walivyomtia moyo na kumuenzi wakati akishikilia wadhifa huo.
Mbali na hayo, Dk Migiro ambaye ameteuliwa na Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon kuwa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya Ukimwi katika Afrika, amesema ameahidi kuendelea kuunga mkono jitihada, misingi na malengo ya Umoja popote pale alipo.
Alisema njia bora ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ni kujenga ubia na ushirikiano wa karibu baina ya Serikali, asasi za kiraia, wafanyabiashara, mashirika ya hisani, taasisi za kitaaluma na watu binafsi.
“Pamoja na muda wangu wa utumishi katika Umoja wa Mataifa kufikia tamati, naamini hakuna tamati katika utekelezaji wa malengo, misingi na maadili ya Umoja wa Mataifa,” alisema Dk Migiro katika tafakuri yake ambayo imechapishwa katika gazeti hili katika ukurasa wa 23 na 24.
“Daima nitaendelea kushukuru na kuthamini kwa dhati jinsi Rais Jakaya Kikwete, Serikali na Watanzania wenzangu walivyonitia moyo na kunienzi katika kipindi chote nilichokuwa Umoja wa Mataifa,” alisema Dk Migiro ambaye kabla ya uteuzi wake kwa UN miaka mitano na nusu iliyopita, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.
Alimshukuru Katibu Mkuu Ban Kimoon kwa kumpa fursa, kumuamini na kushirikiana naye wakati wote wa utumishi alioufanya kwa miaka mitano na nusu na kuwa hiyo ni heshima ya pekee ambayo daima ataienzi.
Alisema bado kuna umasikini duniani, mahitaji ya chakula, changamoto ya kutunza utu na heshima ya binadamu na haja ya kuimarisha amani duniani.
Aidha, alisema anaamini kuwa vijana ni kizazi ambacho kina kila sababu ya kuwa na kiu ya kuishi kwenye dunia yenye utu, usawa, haki na amani, na watauchukulia Umoja huo kuwa mbia wa kuaminika katika kujenga mustakabali wao.
“Zaidi ya yote, sitasahau hisia nilizopata kila nilipokutana na watu wanyonge waliokuwa wanahitaji msaada wa Umoja wa Mataifa,” alieleza.
Aidha, alisema kwa muda wote huo wamefanya mambo mbalimbali ikiwa ni masuala ya maendeleo, uwezeshaji wa
wanawake na usawa wa kijinsia, huduma ya pamoja, afya ya jamii na utawala wa sheria.
“Hii ni mifano michache tu inayojibu hoja za wakosoaji wa Umoja wa Mataifa, ujumbe wangu kwao ni kuwa wanyonge na wenye kutaabika sehemu zote duniani ni mashuhuda na watetezi wakubwa wa Umoja.
Kwa wanyonge na wahitaji walio wengi, Shirika hili ni nguzo ya kutumainiwa katika jitihada zao za kila siku za kujiletea maisha yenye utu na heshima,” alisema Mtanzania na Mwafrika huyo wa kwanza kushika wadhifa huo wa pili kwa ukubwa katika Umoja wa Mataifa.

No comments:
Post a Comment