Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 22, 2012

MSUMBIJI SASA WAANZA KUTENGENEZA DAWA ZA HIV...!

Msumbiji imeanzisha kiwanda cha kutengeneza madawa ya kukabiliana na janga la HIV na Ukimwi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali ni cha kwanza cha aina yake barani Afrika na kimejengwa kwa msaada wa dola milioni 23 kutoka Brazil na dola milioni 4.5 kutoka shirika kubwa la uchimbaji madini nchini humo Vale.
Kuna watu takribani 2.5 wanaougua ugonjwa wa Ukimwi Msumbiji. Idadi hiyo ni sawa na asilimi 12 ya watu wote wa nchi hiyo. Kiwanda hicho cha madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi kimefunguliwa mjini Matola katika sherehe iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais wa Brazil na Waziri wa Viwanda wa Msumbiji Armando Inroga

No comments:

Post a Comment