MRADI wa ujenzi dampo la kisasa wenye thamani ya shilingi
bilioni 3 unofadhiliwa na benki ya dunia katika jiji la Arusha, upo hatari kuyeyuka kufuatia wananchi wa kata ya Muriet
manispaa ya Arusha kugoma kupisha eneo la
mradi huo licha ya kulipwa stahili zao .
Aidha mradi huo ambao
ulikuwa uanze tangu april mwaka jana umeshindwa kuendelea kutokana na mvutano
mkali ulipo kati ya wananchi zaidi ya 200 na manispaa ya jiji la Arusha ,ambapo
wananchi hao wameilalamikia manispaa hiyo kwa kushindwa kuwalipa fidia ya
maeneo yao waliyoyaendeleza ,huku manispaa hiyo ikidai imeshawalipa.
Akizungumzia swala hilo ,
Mkurugenzi wa manispaa ya Arusha, Estomih Changa’h alikiri wananchi hao kuwa
kikwazo cha kuanza kwa mradi huo huku akidai kuwa wafadhili wa mradi huo ambao
tayari walionyesha nia na kuja na kupima katika eneo hilo wameanza kukata tamaa.
Alifafanua kuwa , baada ya
kufanya tathmini ya awali mwaka jana walibaini kuwa wananchi 42 ndio waliopo ndani ya eneo husika la mradi ,hivyo manispaa ya Arusha
ilifanya tathimin na kukubali kuwalipa kiasi cha shilingi milioni 252 kama fidia ya
makazi yao.
‘’tulipofanya tathimini ya
makazi yao tulikubaliana kuwalipa wakazi hao 42,na kila mtu alipigwa picha
akiwa amesimama mbele ya eneo ama nyumba yake,sasa tunasikitika sana kuona
wakiendelea kunga’ng’ania huku kundi lingine la watu zaidi ya 200 wakiibuka
kutaka nao walipwe fidia’’alisema Chang’ah
Alisisitiza kuwa,tayari manispaa
imeshawalipa wananchi 33 kati ya 42 kwa kiwango tofauti na kubaki wananchi tisa
tu ambao walikuja kurubuniwa na kugomea malipo hayo.
Changáh aliongeza kuwa,
baada ya kumaliza kuwalipa fidia wananchi hao, anashangazwa kuibuka kwa kundi lingine
la wananchi zaidi ya mia mbili kuanza kudai kuwa wanahitaji nao kulipwa fidia
za maeneo yao ili kupisha mradi huo wa dampo la kisasa.
Aliongeza kuwa, wananchi
hao wamekuwa wakifika katika ofisi ya manispaa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha
kudai fidia zao ambapo wamekuwa wakijaribu kuwaelewesha na uendesha vikao
kadhaa, lakini wamekuwa wagumu kuelewa .
Hata hivyo Changáh alitumia
fursa hiyo kuwataka wananchi wa mkoa wa Arusha, kuukubali mradi huo na kuunga
mkono kwani ni muhimu sana na utaondoa
tatizo sugu la mlundikano uchafu na hadha ya harufu kali kwa wakazi wa eneo la
Muriet lililopo dambo la sasa.
Aidha alisema mradi huo
utakapokamika utaongeza madhari ya jiji la Arusha kuwa safi na pia utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme pamoja
na kutoa ajira kwa vijana na wakazi wa eneo hilo.
Kwa upande wa wananchi
hao,wamedai kuwa manispaa hiyo imeshindwa kuwalipa fidia na kutumia ubabe
kuwahamisha katika eneo hilo baada ya kuwarubuni wenzao wachache na kuwalipa
fidia ndogo, hatua ambayo wameapa kukwamisha mradi huo kwa kutohama katika eneo
hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya waathirika hao ,Jackson Japhet
alisema kuwa, wao wanachotaka ni kutaka kulipwa fidia stahili ya makazi yao
kwani wengi wa wananchi wamekuwa
wakiishi hapo muda mrefu na wamekuwa na makazi ya kudumu ,hivyo ni ngumu sana
wao kuondoka katika eneo hilo.
Wakizungumza katika kikao
cha hadhara katika eneo hilo la Muriet mwishoni mwa wiki, wameazimia kwenda
mahakamani kusimamisha uanzishaji wa mradi huo hadi manispaa hiyo itakapofanya tathimini upya
kwa kuwashirikisha wananchi hao na kuwalipa fidia stahili bila kuwapunja.
No comments:
Post a Comment