KILIMANJARO watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wanashikiliwa
na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kupora kwa
kutumia silaha za moto katika maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
Mbali na kushikiliwa kwa majambazi hao, pia jeshi la polisi, limefanikiwa kukamata bunduki
mbili aina ya shotgun yenye namba za usajili 13704 ikiwa na risasi tatu, pamoja bunduki aina ya SAR yenye nambari 3811 ikiwa na risasi zake sita.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Moita Koka,
amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kusema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14
majira ya saa 04:00 usiku katika eneo la daraja la Holili tarafa ya Mengwe
wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
Koka alisema watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa
kwa sababu za kiupelelezi wamekuwa wakijihusisha na ujambazi wa kupora kwa
kutumia silaha katika maeneo ya mbalimbali ya wilaya ya Rombo na Himo.
Koka alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya askari
kufanya msako mkali katika maeneo ya Holili kufuatia kuwepo kwa matukio mengi ya
uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha.
Alisema askari hao waliwahoji watuhumiwa hao ambapo waliwaelekeza
walipo walipoficha silaha hizo na polisi
kufanya upekuzi kwenye eneo hilo na kufanikiwa kukuta silaha mbalimbali ikiwemo
bunduki hizo pamoja na mali mbalimbali walizo iba kwenye maduka ya watu.
Aidha alisema jeshi la polisi linaendelea kuwashikilia
watuhumiwa hao kwa upelelzi zaidi na
kwamba iwapo watakutwa na hatia watafikishwa mahakamani ili sheria iweze kufuata mkondo wake.
Koka ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuimarisha vikundi
vya polisi jamii katika maeneo yao ikiwa
ni pamoja na kuwa wepesi kutoa taarifa za siri za uhalifu kwa jeshi la polisi
ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema kabla ya madhara kutokea.
No comments:
Post a Comment