Jiji
la Arusha ni miongoni mwa majiji makumbwa hapa nchini ambayo
yanakabiliwa na foleni kwa nyakati za asubuhi na jioni jambo ambalo
limekuwa likisababisha kero kubwa kwa watumiaji mbalimbali wa barabara
hizo.Miongoni mwa barabara ambayo inaathirika zaidi ni ile ya Old Moshi.
Aidha
barabara ambayo inaongoza kwa kuwa na foleni kubwa ni ile ya Dodoma
ambayo huwa na magari mengi wakati wa kwenda na kurudi majira ya asubuhi
na jioni.
lakini
tatizo kubwa linaloelezwa na watumiaji wa baraba hizo kuwa ni
miundombinu hafifu na barabara zinazoingia na kutoka katikati ya mji
kuwa ni chache. Wadau mbalimbali wamependekeza kuanza mapema mchakato wa
kuzifanyia upanuzi barabara muhimu jijini humo hasa ukizangatia mji
huo unavyo panuka huku shughuli nyingi za utalii zikiongezeka sambamba
na maofisi ya kimataifa hivyo idadi ya watu pamoja na watumiaji wa
magari kuongezeka siku hadi siku.
No comments:
Post a Comment