August 1 2012 Jumatano
jioni kilichoandikwa kwenye website ya club ya soka ya Azam Fc kuhusu mchezaji
wao Mrisho Ngasa kuuzwa ghafla ni hiki, “Biashara na Mjadala wa Mrisho Ngasa
umefungwa leo mchana saa tisa kasorobo baada ya Simba SC kuizidi nguvu Yanga na
kutoa shilingi milioni 25, ofa ya Yanga iliiishia milioni 20″
Azam FC inamtakia kila
la heri na mafanikio mema Mrisho Ngasa kwenye klabu yake mpya ya Simba.
Hayo yote ni maelezo
yaliyotolewa kwenye website ya Azam Fc ambapo mpango wa kumuuza haukuwepo
kabisa, umekuja ghafla baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kagame Cup.
kama bado unashangaa kwa
nini Ngasa ameuzwa mapema hivi nataka kukwambia kwamba juzi yani Jumanne july
31 kwenye website ya Azam kuliandikwa hivi “Hadi hivi sasa Ofa ya Simba ni
shilingi Milioni 25 na Yanga ni Milioni 20, kutokana na hilo Simba wapo kwenye
nafasi kubwa ya kumnyakua Mrisho Ngasa. Kesho ni siku ya Mwisho. Ingawa
tungependa kumuuza Mrisho Ngasa Yanga lakini tutampeleka kwa timu iliyotoa ofa
nzuri zaidi”
Kwenye sentensi nyingine
wakaandika “Lengo la Azam FC lilikuwa ni kumpeleka Mrisho kwenye timu ambayo
atacheza kwa raha na amani kutokana na yeye kuivaa na kuibusu Jezi ya Yanga
siku ambayo Azam FC haikuwa na mchezo na Yanga… Azam FC inaamini kuwa Yanga
ilikuwa Sehemu sahihi kwa Mrisho, lakini uongozi wa Yanga umeonekana kutokuwa
na haja na Mrisho na ndiyo maana umeonekana kukataa kutoa ofa ya maana,
Kutokana na sababu hizo Azam FC italazimika kumuuza Mrisho Ngasa Simba kwani
hatuhitaji kuwa na mchezaji ambaye anafanya vitendo vya kuidharau brand ya Azam
FC ambayo tunajaribu kuijenga” – Azam Fc
Imefahamika kwamba kitendo
cha Ngasa kuivaa na kuibusu jezi ya Yanga ndio kitu pekee kilichowakasirisha
maboss wa club hiyo na kuamua kumuuza mchezaji huyo ambapo Azam walitoa taarifa
za kumuuza mchezaji huyo July 30 2012 na kuandika kwamba “Klabu ya Azam FC
inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa milango iko wazi kwa klabu yoyote kumnunu
mchezaji Mrisho Ngassa kwa gharama ya $ 50,0000″
“Azam FC imefikia hatua
hiyo baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na mapenzi na klabu hiyo na
badala yake kuipenda klabu aliyotoka ya Yanga hivyo uongozi wa klabu unapokea
maombi kwa klabu yoyote inayomuhitaji, Ngassa anauzwa siku chache baada ya
kukubali kuvaa jezi ya Yanga na kuibusu logo ya timu hiyo, baada ya kumalizika
kwa mchezo wa nusu fainali kati ya Azam FC na AS Vita Club ya Congo DRC katika
mashindano ya Kombe la Kagame yaliyomalizika Julai 28 mwaka huu” – Azam Fc
No comments:
Post a Comment