Hii ndio Meza yenye Computer iliyoungua na kusababisha moto.
Hizi ni faili za ofisi ya BUMACO, zilizosalimika baada ya moto huo kufanikiwa kuzimwa na kikosi cha zimamoto Moshi.
Tumaini akiwa Hospitalini St. Joseph akipata matibabu.
Leo majira ya saa saba mchana moto mkubwa umewaka katika jengo la KNCU Moshi na chanzo cha moto huo kimedaiwa ni binti mmoja aliyejulikana kwa Jina la Tumaini Arkyo ambaye King Jofa nilifanya juhudi za kumtafuta ili aweze kunijuza kilichotokea na nilifanikiwa kumkuta katika Hospitali ya St. Joseph iliyopo maeneo ya soweto Moshi. Nilifanikiwa kumuuliza chanzo cha moto naye alinielezea hivi "Mini nilipigiwa simu na mteja wetu akiniomba nikamkatie bima ya gari yake na alinisisitiza sana maana alisema anataka kusafiri kesho, nikatoka na kuelekea ofisini, nilipofika nje ya ofisi ya BUMACO INSURANCE COMPANY LTD. iliyopo ndani ya jengo la KNCU Moshi, nikampigia simu zaidi ya mara tatu mteja huyo na hakupatikana kwenye simu, nikaingia ofisini nikawasha computer ndio moto wa ajabu ukalipuka na mpaka sasa sijui ule moto ulitokea wapi?" mwisho wa kunukuu. Lakini sikuishia hapo nilitaka kuja baada ya kuona moto alichukua hatua gani akajibu "Nilitoka nje na nikiwa kama nimechanganyikiwa na sikuweza hata kutambua kuwa nimeungua mpaka watu niliokuwa naongea nao wakaona moshi ukitokea ndani ya ofisi na wakawa wananishangaa nilivyoungua miguuni, ndio wasamaria wema wakanipakiza kwenye gari na kunileta hospitalini hapa, ila namshukuru Mungu nimeshapata matibabu na ninaendelea vizuri japo Daktari amenishauri nibaki hapa hospitali mpaka kesho ili waendelee kunifanyia vipimo zaidi" mwisho wa kunukuu.. Watu walioshududia moto huo wamekisifu sana kikosi cha zimamoto Moshi jinsi kilivyoweza kufika kwa wakati na kufanikiwa kuuzima moto huo kabla haujaleta madhara makubwa. Mpaka sasa haijajulikana moto umesababisha hasara ya shilingi ngapi?..
No comments:
Post a Comment