Kwa wakazi wa Dar es salaam na waliopo mikoani hii ndio njia
wanayoItumia matapeli kujipatia mali. Utapeli huu ulianza kama utani takribani
miezi mitatu iliyopita na ulianza kama utani lakini kwa sasa umezidi kupamba
moto hasa kwa wakazi wa Dar es Salaak na hususani kwa wanawake. Na mpaka sasa
wanawake zaidi ya wane wamesha report
kuhusu kutapeliwa kwa njia hii ya kupigiwa simu au kufuatwa katika eneo lako la
kazi na watu wasio wajua na kujitambulisha kwao na kuwaeleza mambo mengi
yahusuyo biashara na katika kuhakikisha kuwa wanafanikisha utapeli wao husema
wameagizwa na ndugu, jamaa au rafiki yako wa karibu ambaye wanauhakika unamjua
na baada ya hapo huanza kukuelekeza sehemu ya kwenda kukutana au kumsubiri
rafiki yako huyo walio kutajia huku wakijitahidi kukupumbaza akili ili usiweze kumpigia
simu.. Wakishafika hotelini au kwenye mgahawa hukupa fursa ya kuagiza kinywaji
na hapo ndipo wanapofanikisha adhma yao maana kwenye kinywaji utakacho kiagiza
wenyewe hukiwekea madawa ya kulevywa, unapomaliza kinywaji papo hapo unapoteza
fahamu na matapeli hao huchukua kila ulichonacho na kukupeleka mpaka karibu na
nyumbani kwako na kukutelekeza na unapopelekwa hospitali na kupata matibabu na
kurudi kwenye hali ya kawaida unapompigia mtu uliyetajiwa na matapeli wale kuwa
kuna biashara mnakuja kuifanya mtu huyo hushangaa na kukana kuwafahamu matapeli
hao…
ANGALIZO: Ni vyema kwa yeyote atakaye pata ujumbe huu
amfahamishe na mwenzake ili kumuepusha na matapeli hawa ambao kwa sasa wamezidi
kuwa wajanja sana.
No comments:
Post a Comment