Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 17, 2012

OFISI YA JOFATECH COMPUTERS SERVICE YAVUNJWA NA KUIBIWA...!

 Hii nisehemu ambayo wametumia kupita nakuingia ndani

 Hii ningazi waliotumia kupanda na kuingia ndani wakiwa kwanje

 Hii Pc ni aina ya Dell imetolewa power supply na baadhi ya vifaa vyake vya ndani havipo vilichukuliwa hiyo jana kwenye tukio hilo la wizi.

 Baadhi ya hard disk zilizo salia baada ya vifaa vingine kuibiwa.



Uharibifu uliofanyika kwa baadhi ya vifaa vilivyo salia.

Duka liliopo majengo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro linalojulikana kwa jina la Jofatech Computers Services limevunjwa usiku wa kuamkia leo na kuibiwa computers pamoja na vivaa vya computer ambavyo mpaka sasa hafijajulikana thamani yake..
Mmiliki wa duka hilo anayefahamika kwa jina la Joshua Fanuel au King Jofa amedhibitisha kutokea kwa uhalifu huo ambao mpaka sasa hajajua ni akina nani walihusiika na uhalifu huo ila ameshafikisha taarifa polisi na tayari uchunguzi umeanza kufanyika ili kuweza kubaini walio husika na wizi huo.
             Mtandao huu ulipotaka ulifanikiwa kuongea na King Jofa na aliwaeleza hivi "Mimi nimepigiwa simu leo saa tatu asubui na mfanyakazi wangu na kuniambia kuwa wezi wamevunja na kuiba vitu ofisini, nilishtuka sana maana ni taarifa ambayo sikuitegemea cha kwanza nilikata simu kwanza na kukaa kama dakika kumi na kumpigia tena simu mfanyakazi wangu ili kufahamu zaidi,, alinieleza kilicho tokea na akaniambia yupo kituo cha polisi cha majengo anatoa taarifa ili tuweze kufuatilia zaidi. Niliamua kwenda kituo cha polisi na nilipofika tuliamua kwenda ofisini kuangalia kilichotokea na kurudi polisi kutoa maelezo na tukapewa RB ili kuendelea na uchunguzi tukisaidiana na polisi... kiukweli mpaka sasa nilichoweza kugundua kuwa kimeibiwa ni computer nne, flat screen mbili, na vifaa mbalimbali vya computer pamoja na pesa kidogo zilizokua zimeachwa ofisini"

Swali la mwisho ni je mpaka sasa kuna taarifa zozote umesha zipata za kuashiria au kufahamu walio husika na uhalifu huo? "Hapana maana bado ni mapema sana" alijibu huku akionyesha kuwa katika hali ya masikitiko makubwa sana.

No comments:

Post a Comment