Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini ya kiislam wa Wilaya wa
Mwanga mkoani Kilimanjaro,wakati alipokuwa akiwasili kwenye hafla ya
harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya sekondari ya kiislam
ya Lambo huko Mwanga mkoani Kilimanjaro iliyofanyika mwishoni mwa
wiki.Kushoto ni Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa
akizungumza waumizi wa dini ya kiislam waliohudhulia hafla ya harambee
ya kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya sekondari ya kiislam ya Lambo
huko Mwanga mkoani Kilimanjaro iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Mh
Lowassa alichangia shillingi millioni 10 na kusema Bakwata wilayani
Mwanga ni mfano wa kuigwa kwa kuwekeza katika elimu.Kulia ni Waziri wa
Maji Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiendelea kuchangisha kwenye harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya
Masheikh wa Wilaya ya Mwanga,Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuongoza
harambee hiyo ya kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya sekondari ya
kiislam ya Lambo huko Mwanga mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment