Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa akitoa taarifa kwa waandishi
wa habari (hawapo kwenye picha) ya ajali iliyoua mchungaji wa kanisa la
Pentekoste.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mtu
mmoja amekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa sehemu mbalimbali
za miili yao baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia kisha
kupinduka mkoani Singida.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida Kamishina msaidizi Linus Sinzumwa, amesema
ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku katika eneo la mzunguko
mjini Manyoni barabara kuu ya Dodoma-Mwanza.
Amesema
wakati wa tukio hilo wachungaji wa kanisa la Pentekosti walikuwa
wakisafiri kwa gari ndogo aina ya Land Cruiser yenye namba za usajili
T.531 EAT wakitokea Mwanza kwenye mkutano wa injili, kurejea Dodoma.
Hata
hivyo, amesema kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa mwendo kasi baada
ya kufika eneo la mzunguko Manyoni, dereva wa gari hiyo alishindwa
kuilmudu kabla ya kuacha njia na kupunduka.
Kamanda
Sinzumwa amesema hali hiyo ilisababisha kifo cha mchungaji Jackson
Husena (58) papo hapo huku wachungaji wengine Jonas Chungu, Pasian
Chiwanda na Stephano Ulaya, wakijeruhiwa.
No comments:
Post a Comment