Mkurugenzi
Mtendaji wa NSSF Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi
wa ofisi mpya ya mfuko huo katika eneo la Usa river Wilayani Arumeru.
Mkurugenzi
mwendeshaji wa NSSF Cricentus Magori (mwenye suti nyeusi ) na
katikati ni Mkurugenzi Mkuu Ramadhani Dau wakiingia katika eneo la
uzinduzi.
Wadau
mbalimbali, wafanyakazi na wanachama wa NSSF wakiwa ndani ya jengo hilo
jipya ili kujionea namna ofisi zilivyokamilika tayari kwa huduma (Picha
zote na Story Mahmoud Ahmad – Arusha).
Mfuko
wa hifadhi ya jamii (NSSF) umezindua ofisi mpya katika kata ya Usariver
wilayani Arumeru ikiwa ni moja kati ya kuboresha huduma za wanachama
wake katika wilaya hiyo ili kuweza kuwasogezea huduma wananchi karibu
zaidi.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Bw. Ramadhani Dau
amesema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya ambazo zinaiingizia
michango mingi zaidi katika mfuko huo ambapo amesema kuwa kwa mwezi
huingiza milioni 432 kwa mwezi.
Bw.Dau
ameongeza kuwa mchango huo kwa mwezi ni mkubwa sana kwa kuwa ndani ya
mwaka mzima ni sawa na shilingi biloni tano, hali mbayo inaashiria kuwa
kukiwa na ofisi hiyo karibu kutaongeza idadi ya wananchama wengine wapya
katika mfuko huo.
Aidha
amefafanua kuwa lengo la NSSF kufungua ofisi hiyo ni kuwa karibu na
wanachama ili waweze kuweka michango yao kwa urahisi zaidi na
kuwapunguzia gharama za kufuatilia mafao ambapo hapo awali walikuwa
wanalazimika kufuata huduma zote za mfuko mjini Arusha.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Cricentus Magori amesema kuwa
shughuli ambazo zinafanyika katika wilaya hiyo haswa mashamba makubwa ya
maua ambayo yapo maeneo mbalimbali, shughuli za uchimbaji wa madini
ndio chachu ya kupata michango mingi na wanachama wengi katika wilaya ya
Arumeru.
Bw.
Magori amesema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina wanachama elfu saba ambapo
amesema kuwa wameona ni muhimu kufungua ofisi ili kuwapatia huduma na
kuondoa usumbufu wa kufuata huduma hizo mjini Arusha.
Katika
uzinguzi huo uliofana sana ulifanyika katika kata ya Usa River wilaya
ya Arumeru na kuwashirikisha wafanyakazi na wanachama wa mfuko huo
pamoja na wadau mbalimbali.
No comments:
Post a Comment