Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 15, 2012

WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA KUPIGWA PICHA ZA UCHI WAKATI WA TAMASHA LA FIESTA DODOMA....!

 
Msaanii maafuru wa filamu nchini Tanzania asiyeishiwa na vibweka Wema Sepetu (katikati) akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar kwa nia ya kuomba radhi kwa watanzania kwa niaba yake na msanii mwenzake Aunty Ezekiel kuhusiana na tukio la wao kupigwa picha zilizowaonyesha ‘ndivyo sivyo’ nusu uchi wakati wakijiachia katika Tamasha la Serengeti Fiesta lilipofanyika mkoani Dodoma. Kulia ni Msanii wa Bongo Movie Aunt Ezekiel na kushoto Katibu Mkuu wa TAFF Wilson Makubi.
Msanii Maarufu wa filamu za Bongo Aunty Ezekiel akisisitiza kuwa wao wameumia sana kwa kuonekana kwa picha zile kwa sababu wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi, Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na mashabiki mbalimbali wa kazi zao ambao wanawaheshimu kuliko baadhi ya watu wanavyofikiria.
Wema Sepetu Mbele ya kamera ya MO Blog akiomba radhi na kusema watanzania “ Kiukweli hatujafurahia na tumeumia sana” na tunatumia fursa hii kuomba Msamaha.

Chanzo: www.dewjiblog.com

No comments:

Post a Comment