Kundi linalokuja kwa kasi Mkoani Kilimanjaro Chopper Art's Group ambalo linatarajia kuanza kutengeneza filamu yao ya kwanza inayokwenda kwa jina la GHOST OF MY MOM jana limekamilisha kipengele muhimu baada ya kuipatia Tenda ya kufanya kazi ya kuchukua video na kuhariri filamu hiyo kampuni ya Utengenezaji wa Filamu ya jijini Dar es Salaam UWEZO PRODUCTION iliyo chini ya Mtengenezaji Filamu Maarufu jijini Dar es Salaam. Farid Uwezo.
MKURUGENZI WA KAMPUNI Y GRM INVESTMENT NA MLEZI WA CHOPER ART'S GROUP AKIWEKA SAHIHI KATIKA MKATABA WA MAKUBALIANO YA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA UWEZO VIDEO PRODUCTION
Akisaini mkataba wa tenda hiyo Mlezi na Mdhamini wa wa kundi la Chopper Art's Group Rose Mary Migire ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya GRM INVESTMENT alisema lengo kubwa la kampuni yake kudhamini kikundi hicho ni nia ya dhati nia moyo wa kujituma uliooneshwa na wasanii wa kikundi hicho pamoja na aina ya filamu wanayotarajia kutoa yenye muonekano wa kiafrika.
Naye Farid Uwezo alisema anatarajia kufanya filamu hiyo kwa kiwango cha hali ya juu na kuonesha uwezo wake wote na atadhihirisha kwanini anaitwa UWEZO. Farid Uwezo kupitia kampuni ya Uwezo Production ameweza kufanya kazi mbalimbali na wasanii wengi kama Ray, Odama, Hemed, Marehemu Steven Kanumba na Jb ambapo kwa sasa anamalizia kazi ya Odama kisha atafuata Filamu mpya ya Ray ndipo aanze kazi ya Choper Art's Group.
FARID UWEZO AKIWEKA SAHIHI KATIKA MKATABA WA MAKUBALIANO YA KAZI BAINI YA KAMPUNI YAKE NA CHOPER ART'S GROUP
Choper Art's Group inawakaribisha watu mbalimbali kwa ushauri na hata msaada wa hali na mali ili kukamilisha lengo lao la kutoa filamu yenye ubora. Kwa sasa wanafanya mazoezi katika ukumbi wa Mr. Price City mjini Moshi au wasiliana nao kwa namba +255 759 588680.
FARID UWEZO AKIHESABU FEDHA ALIZOPATIWA ZA KAZI ALIZOPATIWA NA CHOPER ART'S GROUP BAADA YA KUSAINI MKATABA.
No comments:
Post a Comment