CCM MKOA KILIMANJARO YAADHIMISHA MIAKA 36 HAPO JANA TANGU KUZALIWA KWA CHAMA HICHO
Jana katika viwanja vya kata ya Pasua iliyo ndani ya Manispaa
ya Moshi, Kulirindima shamrashamra ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya
kuzaliwa kwa Chama hicho. Akipokea Maandamano makubwa ya wanachama wa CCM
yaliyokuwa yakiongozwa na Kamanda wa Vijana na Mjumbe wa NEC moshi mjini Ndugu
Agrey Mareale, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. LEonidas Gama alisema Furaha ya
Maadhimisho haya iambatane na Utekelezaji wa Sera ya chama cha mapinduzi ya
kulinda amani na kuchochea Maendeleo na yeye kama Mwakilishi wa Serikali ya CCM
ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro atahakikisha anasimamia hilo.
Katibu wa CCM mkoa kilimanjaro Mh Kazidi, Akimtambulisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Mh. Idi Juma
Hata hivyo Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro ndugu Kazidi
aliongeza kwa kusema CCM hawatojibu matusi yanayotolewa na CHADEMA dhidi yao na
akamuomba mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kutojibu matusi anayotukanwa kila mara
katika mikutano yao kwa sababu tu anasimamia vyema fedha za wananchi wa moshi
zisitumiwe kinyume na Taratibu.
Mwenyekiti wa CCM mkoa kilimanjaro akipokea kadi za wanachama wapya wanaotoka vyama vya upinzani hapo jana
Katibu huyo ameweza kuelezea mambo mbalimbali yaliyofanywa
na serikali ya ccm katika mkoa wa Kilimanjaro kama kujenga barabara, kukarabati
barabara, kujenga shule za kata, Zahanati na hata kuwezesha kuwapa elimu ya
ujasiria mali vikundi mbalimbali ili kuweza kujiajiri ambapo moja ya utekelezaji
wa ilani ya ccm ni Sacoss mbambali zilizofunguliwa.
Pia waliweza kupokea vikundi mbali vya vijana na wakina mama
waliweza kurudisha kadi za Upinzani na kuahidi kufanya kazi ya kutoa elimu
dhidi ya uzalendo kwa wananchi wanaotangaziwa siasa za uvunjaji wa amani.
No comments:
Post a Comment