Maandamano hayo yanayoratibiwa na CHADEMA lakini pia yakishirikisha vyama vingine vya siasa yana lengo la kupinga namna bunge linavyoendeshwa na viongozi wa bunge. Lengo ni kuwashitaka viongozi hao kwa umma katika mkutano utakaofanyika baada ya maandamano hayo. Maandamano yamepangwa kuanzia Ubungo - TAZARA hadi Temeke ambako yatasitishwa kwa kufanyika mkutano mkubwa wa hadhara.
Katika taarifa yao polisi wamesema hawaruhusu maandamano isipokuwa mkutano wa hadhara tu ndio umeruhusiwa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Temeke bwana Kiondo amesema barua ya CHADEMA ya kuomba kibali cha maandamano imekaa "kiujanja ujanja".
Kamanda huyo amedai CHADEMA hawana maslahi na nchii hii na wanataka kuleta vurugu tu na kusababishia watu hasara na hata mauaji. Amekumbusha vurugu zilizotokea huko Mtwara na kutaka zisitokee hapa tena.
Source:Nipashe
No comments:
Post a Comment