TANZANIA
kupitia shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) limefanikiwa kuingia katika
maajabu saba katika bara la Afrika kupitia vivutio vyake vitatu bora
vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na
Hifradhi ya Serengeti ambavyo viliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko
nchi zingine hali ambayo itafanya Sekta ya utalii hapa nchini iweze
kukua na kuimarika
Akitangaza matokeo hayo jana mjini hapa, rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani,alisema kuwa katika kinyanganyiro hicho Tanzania imepata ushindi kwa kuwa vivutio vya aina yake.
Alitaja vivutio hivyo kuwa ni Pamoja na Mlima Kilimanjaro,hifadhi ya Serengeti pamoja na bonde la Ngorongoro ambapo vivutio hivyo viliweza kupigiwa kura nyingi sana na hivyo kuvipa ushindi wa hali ya juu huku ndani ya vivutio hivyo kuna maajabu ya aina mbalimbali ambavyo havipatikani popote barani Afrika na duniani kwa ujumla
“leo nina furahi kutangaza kuwa Tanzania imeingia ndani ya maajabu saba na hivyo basi hii ni kama changamoto ya kuhakikisha kuwa bado mnaendelea kufanya viendelee kukua na kuinarika zaidi ili hata wakati mwingine muwe na vivutio vingi zaidi’aliongeza Dkt Imler.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema kuwa nchi za Afrika zina vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii huo.
Alisema anaamini kutokana na sifa ambayo Tanzania imeipata kupitia vivutio vyake vitatu itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la taifa.
Aliongeza kuwa ndani ya Nchi ya Tanzania kwa sasa wamejiwekea juhudi za makusudi kuanzia ngazi ya kitaifa ambapo kupitia ngazi mbalimbali wataweza kuharakisha maendeleo ya utalii hususani utalii ili maajabu mbalimbali ya Tanzania yaweze kufahamika duniani.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema ushindi huo ni historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la Watanzania wote kujivunia.
kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa hapa nchini(TANAPA)Alan Kijazi alisema kuwa wanatarajia mapato kuongezeka hasa katika mlima Kilimanjaro,bonde la Ngorongoro, na hifadhi za Serengeti kwa kuwa vivutio hivyo vimetangazwa rasmi kama vivutio venye maajabu ya kutosha
Alisema Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na Watanzania waendelee kuutunza, Ngorongoro alisema kuwa imeshinda kwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven: simba, tembo, viboko, nyati, vifaru, sokwe na mamba.
Kijazi aliongeza kuwa pamoja na kutangazwa kwa vivutio hivyo lakini bado TANAPA limejiwekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanaendeleza shuguli za utalii hapa nchini ingawaje bado kuna changamoto kubwa sana kwenye masuala ya utalii wa ndani
Rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani akitangaza matokeo hayo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo akihutubia mara baada ya kutangazwa kwa vivutio hivyo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
No comments:
Post a Comment