Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, April 21, 2013

HALIMA KASSIM 'HK' APATA SHAVU BBC...!

Halima Kassim "HK" akiwa katika ofisi mpya.

TAKRIBANI zaidi ya mwezi mmoja tangu ilipotoweka sauti ya dhahabu iliyokuwa imezoeleka kwenye masikio ya wengi sauti hiyo ilikua ikisikika kutoka kwenye kituo cha Radio Kili FM ya mjini moshi ilikua ni sauti iliyosifiwa na wasikilizaji wengi sana kwa kuwa sauti hiyo ilikuwa ya kipekee na yenye kusikika kwa umahiri wa hali ya juu, ambapo kwa wakazi wa mikoa ya kaskazini mwa Tanzania (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) watakua wanaikumbuka na wataendelea kuikumbuka sana sauti hiyo ya mwanadada Halima Kasimu maarufu kama HK.

Lakini ghafla sauti ile ilitoweka pasipo kujulikana ilipoelekea na watu wengi wamekua wakijiuliza maswali ambayo mpaka sasa ni wachache tu walio na ukweli kuhusiana na mwanadada huyu alipo kwa sasa. Chanzo chetu makini cha www.kingjofa.blogspot.com
kilifanya juhudi za kutaka kufahamu alipoelekea na ni sababu gani zilizo msababisha kuwepo huko ambako hapajulikani na pia kwa nini aliondoka bila hata kuwaaga waliokua wasikilizaji wake. Chanzo chetu kilifanikiwa kumpata HK na kufanya nae mahojiano mafupi kwa njia ya simu.

Chanzo chetu: Habari za saizi?
HK: Salama, nani anaongea?
Chanzo chetu: Naongea na Halima Kassim maarufu kama HK?
HK: Mh! Ndio kwani wewe nani?
Chanzo chetu: Unapatikana wapi kwa sasa maana ni muda mrefu sana hatujakusikia radioni?
HK: Ndugu yangu kama hutaki kusema wewe ni nani, unategemea mimi nikujibu maswali yako kweli?
Chanzo chetu: Ok.. mimi ni mmoja wa wanahabari na pia nahusika na blog ya www.kingjofa.blogspot.com, kama unakumbuka nilishawahi kuku tafuta kipindi flani ulipokua likizo.

HK: Oh! Vipi ndugu yangu upo? Naona leo umeamua kunisalimia.
Chanzo chetu: Kwanini uliamua kuondoka kimya kimya bila hata kuaga?
HK: Mh! Kiukweli sikuweza kumuaga kila mtu jamani.
Chanzo chetu: Na ni sababu zipi zilizokusababisha ukahama katika kituo cha Kili FM radio na kwenda huko uliko kwa sasa?
HK: Nadhani ni katika kutafuta maisha zaidi tu ndugu yangu, ila sijaondoka Kili fm, kwa ubaya na bado nawapenda sana, maana Kili Fm, ndiyo iliyonikuza mpaka hapa nilipo sasa hivi, na siku zote nitawaheshimu sana waliokua wafanyakazi wenzangu na hata uongozi mzima wa radio Kili Fm.

Chanzo chetu: Ok. Nadhani wengi wangependa kufahamu upo wapi kwa sasa?
HK: Ooh ok ndugu yangu kiukweli sasa hivi nafanya kazi na BBC (BBC MEDIA ACTION)
Chanzo chetu: Ni changamoto gani unazokutana nazo huko uliko kwa sasa?
HK: Changamoto kubwa ni utofauti katika kazi, kwakua kuna baadhi ya vitu nilikua nafanya ila vilikua vinapaswa kufanyika kwa umakini zaidi, ila baada ya kufika huku sasa inabidi iwe kama kujifunza baadhi ya vitu tena, ila namshukuru mungu kwa haraka nimeweza kukabiliana navyo kwa maana kwamba nimeweza kuvielewa kwa haraka. Kwani hata kufika hapa haikua rahisi, ila ni juhudi ya kazi na heshima pia.
Chanzo Chetu: Unapo sema vitu vilikua vinapaswa kufanyika kwa umakini una maanisha nini?
HK: Oh! Mfano katika maswala ya habari, huku niliko kwa sasa habari mpaka zitoke zinapaswa kua na uhakika mkubwa sana na hata ikiwezekana anae husika katika habari hiyo asikike na uhalisi uwepo, hivyo habari haiwezi kutoka hivi hivi tu bila uhakika mkubwa sana, la si hivyo ni bora habari hiyo isitoke.
Chanzo chetu: Mbona kuna habari kwamba umeolewa na mume wako ameamua uwe mama wa nyumbani?
HK: Hhahhaa! Umepata wapi hizo habari?
Chanzo chetu: Ningefurahi zaidi kama ungenijibu kwanza Hk.
HK: Ni kitu kinachonishangaza ndio maana inabidi niulize, hapana mimi sijaolewa na muda wa jambo hilo bado kwa sasa. Hivyo sasa hivi kazi kwa sana tu ndugu yangu.
Chanzo chetu: Nini matarajio yako ya baadae?
HK: Mtarajio yangu ni kufika mbali hata zaidi ya hapa nilipo, hata hivyo namshukuru m’mungu sana mpaka hapa nilipofika kwa sasa kwakua kwa upande wangu si hatua ndogo. Naishukuru sana familia yangu na marafiki zangu wote waliokua na mimi katika hali zote.
Chanzo chetu: Sasa una waambia nini wasikilizaji wako/mashabiki wako waliozoea kukusikiliza na kwa sasa hawakusikii tena?
HK: Mi napenda tu kuwaambia kua si mwisho wa kunisikia, japo haitakua katika sehemu walio izoea ila watanisikia sana tu. Pia nawapenda sana kwani wao wanamchango mkubwa sana kwangu mpaka mimi kufika hapa nilipo leo hii.
Chanzo chetu: Nashukuru sana kwa muda wako pia nakushukuru kwa kujibu maswali yaliyokua yanawasumbua wengi vichwa.
HK: Nakushukuru sana pia, ahsante kwa kunikumbuka vilevile.

No comments:

Post a Comment