Msanii wa Muziki wa kizazi kipya anayekuja kwa kasi Tanzania
JAILUN anayetamba katika vituo vingi vya Radio na TV na wimbo wake unaokwenda
kwa jina la ANAKUIBIA aliomshirikisha NEIBA anatarajia kuachia Video ya Wimbo
wake Mpya Unaokwenda kwa Jina la STAR aliomshirikisha NASEEB ABDUL aka DIAMOND.
Akipiga Story na Shushushu wa Kingjofa Jailun amesema Video
hiyo itakua moto wa kuotea mbali kwa kuwa huko ndani wameepotezana kuanzia
mavazi mpaka style za kucheza. Akizungumzia Wimbo huo alio mshirikisha Diamond amesema ilikuwa
vigumu kumpata Diamond na kuweza kufanya nae kazi lakini alisema Diamond ni mtu
mwelewa na pia wametoka mbali wameweza kufanya show Boma na pale Moshi mkoani
Kilimanjaro. Jailun yupo na wenzake Rich Mavocco,Timbulo,Sam Waukweli na Dayna
kwa meneja wao Papaa Misifa huku yeye akiwa chini ya mameneja wawili ambao ni
Papaa Misifa na Man Ngereza.
Jailun akimzungumzia NGEREZA amesema Ngereza ni meneja wake
ambae wametoka mbali tangu kipindi Jailun akiwa anaishi Boma Wilaya ya Hai
lakini yeye ni mzaliwa wa Arusha na kwa sasa yupo Dar es salaam akifanya kazi
ya muziki.
Alizidi kufunguka kuhusiana na Meneja wake huyo Jailun
amesema kuwa Ngereza aliweza kusababisha yeye kurekodi wimbo wa Nalia na wewe
ambao aliufanya kwa Mazuu pale Mazuu Records.
Akizungumzia kuhusu Muziki
Amesema Muziki uko kwenye damu na anahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili
aweza kuutangaza vema mziki wa Tanzania na amesisitiza kuwa muziki sio uhuni
bali ni kazi kama kazi zilivyo kazi nyingine.
Haya sasa mwenye macho na atazame Jailun huyooo anakuja
kwenye kichupa……!
No comments:
Post a Comment