Somebody please tell Madee kuwa Hip Hop inauza sana. Kwa mujibu wa Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana
FA ambaye ni mmoja kati ya wasanii wakongwe wa Hip Pop nchini Tanzania leo ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la "Kama Zamani" kwa mujibu wa maelezo yake amekiri kwa kusema hivi
karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza
miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni kumi na nane (18,000,000).
Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa
tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo
chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili
watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.
Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.
No comments:
Post a Comment