MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi zao.
Gama alisema hayo akiwataka kuepuka kufanya kazi zitakazowaingiza
kwenye mikwaruzo huku akiziagiza taasisi za umma kushirikiana na
waandishi wa habari ili kuipa jamii haki yake ya msingi.
Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa
habari, taasisi mbalimbali zilizoko mkoani Kilimanjaro, wakuu wa wilaya,
wakurugenzi na taasisi za dini, vyuo vinavyofundisha uandishi wa habari
vilivyopo mkoani humo na waandishi wa habari katika kongamano la
wanahabari.
Kongamano hilo lililenga kujadili changamoto zinazowakabili wanahabari na maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema mwandishi wa habari anayo nafasi ya kusimamisha nchi na
kuibomoa endepo hatazingatia maadili yao huku akisisitizia suala la
taasisi mbalimbali kutoa ushirikiano na wanahabari mkoani humo.
“Nafahamu wazi kwamba mnazo changamoto nyingi, ninaloweza kusema ni
taasisi za umma kuhakikisha zinawapa ushirikiano na kutosha.
“Hata Rais wa nchi ametoa agizo kwa taasisi zote kutoa habari kwa
wanahabari; zingatieni maadili ya kazi zenu na msife moyo katika
utendaji wenu,” alisema Gama.
Naye mwenyekiti wa klabu hiyo mkoani Kilimanjaro Rodrick Makundi
alitaja changamoto wanazokumbana nazo wanahabari kuwa ni mazingira
magumu ya kazi na kukosa ushirikiano kutoka kwa wadau.
Katika risala hiyo Makundi alisema sh milioni 71.9 zinahitajika ili
kukamilisha ujenzi wa kitega uchumi cha waandishi ikiwemo kuanzisha
Saccos yao.
Akiwasilisha mada yake, juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa
habari meneja wa Redio Kibo, Abdalah Hussein, alisema waandishi wengi
hawana uhakika wa ajira na kwamba wanaishi kwa hofu kutokana na vitendo
wanavyofanyiwa vya unyanyasaji na mauaji.
No comments:
Post a Comment