JINSI YA KUTUMA MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA..!

YAH: MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA
Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert
Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa
maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya
kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini
Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar
es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya
Maziko.
Mpaka sasa ushirikiano
tulioupata ni kampuni ya Clouds Media Group ambayo imebeba jukumu la
kusafirisha mwili wa marehemu kutoka South Africa mpaka Tanzani, Bongo
Records wameshachangia shilling milion 5 na Push Mobile wametoa million
5. Kamati inaomba wizara husika, mashirika, makampuni pamoja na watu
binafsi kutoa michango yao katika kukamilisha jukumu la kumhifadhi
katika nyumb yake ya milele ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha.
Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:
Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738
Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB
Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanganguli shukrani za dhati
No comments:
Post a Comment