LEO ndio siku ya wadau wanaopenda urembo kushuhudia mlimbwende wa Redds Miss Moshi 2013 akinyakua taji pale Aventure Africa mjini Moshi. Kinyang'anyiro hicho ambacho kimekua gumzo mitaani na pia watu kugubikwa na maswali mengi sana kutokana na jinsi ambavyo wamezoea kuwaona kina dada wengi wa moshi wakiwa na maumbile ya miss bantu lakini inapofikia wakati wa kuwasaka mamiss wakwenda kuuwakilisha mkoa wa kilimanjaro kwenye mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa, kina dada hao hujitokeza kwa wingi na wakiwa kwenye muonekano mzuri na wakuvutia.
Chanzo chetu makini cha mtandao huu wa kingjofa.blogspot.com kilifanikiwa kuzungumza na
mratibu wa mashindano hayo Mkurugenzi
wa kampuni ya New Vision Plan inayohusika na kazi za kuandaa mashindano
ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya walibwende wapatao 19 wapo tayari kuchuana vikali maana kila mlimbwende anavigezo vya kushinda kwenye kinyang'anyiro hicho cha kumsaka Miss Moshi. Warembo hao waliofanyia mazoezi katika ukumbi wa aventure na leo hii ndio siku ya kutimua vumbi katika ukumbi huo. Na mpaka sasa kila kitu kinakwenda
sawa.
Katika shindano hilo ambalo wadhamini wukuu ni Redds na kampuni ya Panone and Company Limited na wadhamini wengine ni kama Baba G na Zoom Net Printers ambapo kwa upande wa burudani atakuwepo msanii mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine kutoka Moshi.. Moses Komba alisema kwa taratibu za kuingia Kwenye ukumbi wa Aventure Africa utakua kama ifuatavyo kwa viti vya dhahabu vitakuwa sh. 50,000, viti vya Silver vitakuwa ni sh. 30,000 na
viti vya kawaida ni sh. 15,000.
No comments:
Post a Comment