Rais Barack Obama wa Marekani anatarajia kutembelea bara la Afrika mwezi ujao (Juni) ambapo atatembelea mataifa ya Senegal, Afrika kusini na Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Ikulu ya Rais nchini Marekani Jay Carney, raisi Obama amepangiwa kufanya ziara hiyo kati ya tarehe 28 mwezi Juni hadi tarehe 3 mwezi Julai ambako atakutana na viongozi wa serikali, biashara na wa mashirika ya kijamii kwa lengo la kuhimiza amani na ustawi wa bara Afrika.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Raisi huyo wa Marekani atasisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na nchi za Afrika ikiwemo kupanua ukuaji wa kiuchumi, uwekezaji na biashara pamoja na kuboresha asasi za kidemokrasia.
Mara ya mwisho kwa raisi Obama kutembelea nchi ya bara la Afrika ni mwaka 2009 alipozuru Ghana.
No comments:
Post a Comment