Kundi la sanaa la Filamu mkoa kilimanjaro Choper Art’s Group
leo limekutana pamoja katika mkutano wao mkuu wa Mwaka ambao ulikuana agenda
mbalimbali ikiwemo viongozi kutoa mapato na matumizi ya kikundi katika muda wa
utengenezaji wa Film yao ya Mom’s Ghost ambayo wametengeneza mwezi wa pili mwaka huu.
MWENYEKITI WA CHOPA ART'S GROUP AKIMTULIZA MMOJA WA VIONGOZI WA KUNDI HILO.
Wakati Mwenyekiti wa kikundi hicho aitwaye George Migire akitoa
mapato na matumizi ya kikundi hicho uliibuka mzozo mkubwa wa matumizi ya kiasi
cha shilingi elfu sitini tu. Haapo ndipo mambo mengi yalipoibuka baada ya siri
kubwa kuibuliwa kuwa kiongozi mmoja wa kikundi hicho kutumia fedha hizo kwa
kwenda mganga kwa ajili ya kukinga kundi hilo.
HUYU NDIYE KIONGOZI ANAYETUHUMIWA KUTUMIA
PESA KWENDA KWA MGANGA
King Jofa akizungumza na Kiongozi huyo anayesadikiwa kutumia
fedha hizo kwa ajili ya kwenda kwa Mganga kuhusiana na tuhuma hizo alipinga
vikali na kusema alitumia fedha hizo kwa ajili ya mambo ya ndani ya kikundi na
alirudisha stakabadhi kwa muhasibu wa kikundi.
Haya sasa mambo ndio hayo kumbe makundi yanaendaga kwa
waganga ili wawe juuu.
No comments:
Post a Comment