Alvin
Walter Makundi ni kijana mdogo wa Kitanzania anayeishi na wazazi wake
nchini Singapore. Akiwa na umri wa miaka 14 na mwanafunzi wa kidato cha
pili huko Singapore, tayari ameshatumbukiza jina lake katika orodha ya
wataalamu wa application katika moja ya makampuni makubwa duniani ya
kutengeneza simu za mkononi ya NOKIA, ambapo anatengeneza applications
ambazo anazituma katika kampuni hiyo ambayo nayo bila hiana huitumia.
Kwa idhini ya mama yake. Globu ya Jamii ilipata fursa ya kuongea naye
kuhusu hayo maajabu anayoyafanya. Msikilize. hapo chini...
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Walter P. Makundi, ambaye ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Singapore siku alipokutana
na kuzungumza nao. Bw. Makundi, ambaye ni Meneja mradi wa kampuni kubwa
ya ujenzi ya APCO PTE LTD ya hapo Singapore, ndiye baba mzazi wa Alvin.
Kulia kwake ni mkewe, Mama Alvin.
Chini Rais Kikwete akisalimiana na Alvin ambaye aliongozana na mama yake pamoja na dada kuja kumuaga wakati Rais akiondoka Singapore usiku huu.
Chini Rais Kikwete akisalimiana na Alvin ambaye aliongozana na mama yake pamoja na dada kuja kumuaga wakati Rais akiondoka Singapore usiku huu.
No comments:
Post a Comment