Kama nchi, Tanzania imesaidiwa kwa kiasi kikubwa na Marekani kupitia miradi mbalimbali Dar es Salaam.
Watanzania wanasubiri kwa hamu ujio wa Rais Barrack Obama kuwa utakuwa ni neema katika harakati za kujiletea maendeleo.
Ni heshima kubwa kama taifa kupokea ugeni mzito wa kiongozi wa dola lenye nguvu zaidi duniani.
Kumbuka mwezi Machi Tanzania ilipokea ugeni wa
Rais Xi Jinping wa China, ambayo katika siku za karibuni imekuwa na
nguvu za kutisha katika medani ya uchumi duniani.
China ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania,
lakini katika miaka ya karibuni Marekani imetoa fedha nyingi za misaada
na kuanzisha miradi mikubwa ya kuisaidia Tanzania.
Marekani ni kati ya washirika wakubwa wa maendeleo
kwa Tanzania kwani katika mwaka 2012 ilimwaga misaada yenye thamani
ya Dola750 milioni (Sh1.2 trilioni) kusaidia shughuli za maendeleo.
Nchi hiyo kupitia mfuko wa Global Fund imekuwa ikigharamia kampeni za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.
Global Fund inafanya kazi kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa Mataifa (UN).
Pia, kuna miradi mbalimbali ya kilimo cha
umwagiliaji, elimu, ulinzi na masuala ya ushauri katika usimamizi wa
fedha. Shirika la Maendeleo la Marekani (Usaid) lilitoa Dola 350
milioni (Sh558 bilioni) kwa mwaka 2012 kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia, limemwaga kiasi kingine cha Dola10.5 milioni
(Sh16 bilioni) kwa ajili ya ujenzi wa sehemu za kuhifadhia dawa kwa
Tanzania Bara na Zanzibar.
Usaid, pia imekuwa ikisaidia katika harakati za
kuinua uelewa wa kinamama katika kutambua haki zao. Tayari, watu wapatao
23,000 wamenufaika kutokana na mpango huo.
Shirika la Millenium Challenge-MCC
No comments:
Post a Comment