Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live Joyce Kiria
amepatwa na msiba baada ya baba yake mzazi aliyefariki jana mkoani Tanga
alipokuwa akiishi.
Katika taarifa tulizozipata kupitia ukurasa wa facebook wa kituo cha television cha EATV Joyce aliandika
“Leo ni siku nyingine ya historia kwenye maisha yangu baada ya
baba yangu Michael Francis Iwambo Kiria wa Kibosho Dakau Nganyeni
kufariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi. Kesho (leo) ni safari
ya kuelekea Moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Im speechless... R.I.P MY DAD"
Joyce kiria ni mmoja wa wadau wakubwa sana wa filamu nchini, na
ni mtu aliyetoa na mchango wa pekee katika kukuza tasnia ya filamu
nchini kupitia kipindi chake cha bongo movies kabla hajaanza kutangaza
kipindi cha wanawake live kupitia kituo hicho hicho cha EATV
No comments:
Post a Comment