Wema Isaac Sepetu akiwa na Martin Kadinda.
Kwa mujibu wa chanzo makini, ishu ilianzia mbali na kusababisha hali
kuwa tete kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kuibua gumzo la aina
yake huku mashabiki wa Wema wakidai yao ni macho tu, kuona nini
kitakachojiri.Chanzo hicho kilitiririka kuwa ‘sosi’ ya kutibuana kwao ni baada ya Kadinda kutundika picha ya nyumba yake akiwa amepaka rangi mpya ambapo baadhi ya watu walimpongeza lakini Wema yeye akaguna bila kusifia kama wengine walivyofanya.
Mpashaji wetu aliendelea kutonya kuwa kitendo cha Madam kuguna kilimuumiza Kadinda na kuanza kumwandikia maneno ambayo yalionekana hayakumpendeza Wema.
“Nilijua tu una kiroho na roho ya hasidi iliyojaa uzandiki,” aliandika Kadinda akimjibu Wema.
Ilidaiwa kuwa maneno hayo yalimpandisha hasira Wema na kuamua kumtahadharisha meneja wake huyo kuwa asimwambie maneno ya aina hiyo katika mtandao wa kijamii unaosomwa na wengi.
“Please don’t talk to me like dat on social network (tafadhali usizungumze na mimi hivyo kwenye mtandao wa kijamii),” aliandika Wema.
Mtoa habari wetu aliendelea kumwaga ‘unga’ kuwa baada ya ujumbe huo kumfikia Kadinda naye alijibu mashambulizi kwa kumwandikia Wema: “Umezoea kuogopwa…anyway cut it short (basi yaishe).”
Ilisemekana kuwa baada ya Kadinda kuandika hivyo, wadau mbalimbali kwenye mtandao huo waliwasihi kuweka tofauti zao pembeni au wazimalize wenyewe na siyo kubishana mtandaoni na kufaidisha wasiohusika.
Baada ya habari hizo kutua kwenye ‘deski’ la gazeti hili, mwanahabari wetu aliwatafuta wahusika kwa njia ya simu ambapo Kadinda alipopatikana na kuulizwa juu ya kutibuana na Madam, alikiri kutofautiana na Wema lakini akadai walishaweka mambo sawa.
“Ni kawaida, hata vikombe vikikaa sehemu moja hugongana lakini namshukuru Mungu kwa sasa tupo sawa,” alisema Kadinda anayemiliki lebo ya mavazi ya Single Button.
Kwa upande wa Wema alipoulizwa juu ya ishu hiyo, alicheka na kusema kuwa wao ni binadamu na si malaika hivyo kukwaruzana ni jambo la kawaida.
“Umenichekesha sana, unajua sisi ni binadamu eeeh… siyo malaika, hayo mambo yaliisha siku ileile na hapa baada ya dakika kumi anakuja (Kadinda) kwa ajili ya kupata chakula cha mchana,” alisema Wema
No comments:
Post a Comment