Yule mwanamke-mwanaume wa Marekani ambaye alijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya picha yake akiwa na mimba huku akiwa na midevu kusambaa duniani amerudi tena kwenye vichwa vya habari mwaka huu baada ya kujifungua mtoto wa pili. Thomas Beatie, au maarufu kama 'Mwanaume Mjamzito' amerudi tena kwenye vichwa vya habari vya magazeti baada kujifungua kwa mara ya pili mtoto wa kiume jana asubuhi.
Picha za Thomas akiwa na madevu kibao huku akiwa na tumbo kubwa la ujauzito zilikuwa maarufu sana duniani mwaka jana kiasi cha kumfanya Thomas atajwe kama mwanaume wa kwanza kupata ujauzito.
Thomas anaishi na mkewe Nancy ambaye ndiye atakayekuwa akimnyonyesha mtoto wao mpya kama alivyofanya kwa mtoto wao wa kwanza wa kike anayeitwa Susan Juliette aliyezaliwa mwezi juni mwaka jana.
Thomas alizaliwa kama mwanamke lakini baadae alibadilisha jinsia kuwa mwanaume na kufanya upasuaji wa kuondoa matiti yake huku akitumia madawa ya homone za kiume yaliyomfanya awe na madevu kama mwanaume.
Thomas hakufanya upasuaji wa kuondoa uke wake hali ambayo ilimwezesha kupata ujauzito wa mtoto wake wa kwanza baada ya kupandikizwa mbegu za kiume.
Thomas ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 35 alisema kuwa aliamua kuzaa mtoto baada ya mke wake Nancy mwenye umri wa miaka 45 kutokuwa na uwezo wa kushika ujauzito.
"Kuwa na mtoto hakuangalii kuwa wewe ni mwanamke au mwanamme, mimi pia ni binadamu na ninahitaji kuwa na mtoto" alisema Thomas.
No comments:
Post a Comment