Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Profesa
Tolly Mbwete amesema kuwa walichelewa kufanya mawasiliano na vyombo
vinavyohusika ili kupata fursa ya kumkabidhi Rais wa Marekani, Barack
Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kama walivyokuwa wamepanga.
Profesa Mbwete akizungumza kwa njia ya simu alisema kuwa, ingawa Rais Obama ameondoka nchini bado wana njia mbili za kuweza kumkabidhi cheti ikiwa ni ishara ya kumtunuku shahada hiyo.
“Yule ni mtu mkubwa bwana ingetakiwa tufanye mawasiliano ya kupata
nafasi kumkabidhi kwa miezi mitatu kabla, hata hivyo hiyo shahada kwa
maana halisi tulishampa kwa sababu mkuu wa chuo ndiye mwenye mamlaka ya
kuitoa, kilichokuwa kikisubiriwa ni kumkabidhi cheti tu na yeye atoe
hotuba ya kuikubali,” alisema Profesa Mbwete.
Anasema kuwa,
chuo hicho kitawasiliana na Ubalozi wa Marekani nchini ili kuona njia
itakayotumiwa katika kumalizia mchakato huo.
“Kwa sasa kuna
njia mbili za kumabidhi, sisi tunaweza kwenda ama tunaweza kukituma
cheti hicho kupitia ubalozi na yeye akatuma hotuba yake,” alisema
Profesa Mbwete.
No comments:
Post a Comment