Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo, European Network on Debt and Development (Eurodad) watafanya
ziara ya kiuchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za
Ulaya kuanzia tarehe 20 Oktoba mpaka tarehe 5 Novemba mwaka 2013.
Uchunguzi huo utaendeshwa na wataalamu waliobobea wa masuala ya kodi na
maendeleo. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Bunge
la Tanzania Zitto Zuberi Kabwe ameteuliwa kuongoza Jopo la uchunguzi
huo.
Eurodad
ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 48 kutoka nchi 19
za Ulaya ambayo yanajihusisha na masuala ya kufutia madeni nchi
zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki. Mashirika haya
yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji
kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea. Zitto
amekuwa mmoja wa wabunge wanaosimamia hoja ya kutaka Watanzania
waliotorosha fedha kwenda nje warejeshe na kufunguliwa mashtaka. Mwaka
2012 aliwasilisha hoja binafsi Bungeni na kupitishwa kuwa Azimio la
Bunge ya kutaka uchunguzi kuhusu utoroshwaji wa fedha na kufichwa nje
kama Uswiss. Kikosi Kazi cha Serikali kutekeleza Azimio hilo la Bunge
kinatarajia kuwasilisha taarifa yake katika Mkutano wa Kumi na Sita wa
Bunge. Siku ya Jumatatu tarehe 21 Oktoba Zitto atakutana na Waziri wa
Fedha wa Uswiss na maafisa wa mabenki na asasi zisizo za kiserikali
zilizopo jijini Geneva. Pia Zitto atahudhuria mkutano wa Kamati ya Kodi
ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za
kimataifa ili kuzuia unyonyaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na
Makampuni makubwa ya Kimataifa.
Baada
ya Geneva Zitto atatembelea nchi za Luxembourg na Brussels kabla ya
kwenda Norway ambapo atamalizia ziara yake kwa Jopo la Wataalamu wa
masuala ya kodi na Maendeleo kuandika taarifa maalumu yenye mapendekezo
kuhusu kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika.
Zitto
atakwenda jijini London kutoa mada kuhusu masuala ya kodi za kimataifa
katika mkutano wa Uwazi (Open Government Partnership). Mwenyekiti wa PAC
Tanzania atafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa PAC Uingereza Bi Margaret
Eve Hodge, Lady Hodge MBE, PC, MP kuhusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano wa mabunge mawili na kuendeleza wito wake kwa makampuni ya
kimataifa kulipa kodi zao barani Afrika na kuacha tabia ya kutumia ‘Tax
Havens’ kukwepa kodi na kufukarisha nchi za Kiafrika.
Zitto invited to annual OGP Summit
The
Kigoma North Member of Parliament and Chairman of the Public Accounts
Committee (PAC), Hon Zitto Kabwe has been invited for the annual Open
Government Partnership (OGP) Forum which kicks off in London at the end
of the month.
The
OGP Summit is a chance to promote tax and illicit issues to new
audiences, to encourage new commitments in country action plans.
Hon
Zitto, who also serves as Deputy Leader of Official Opposition in the
Parliament, will serve in the panel which will discuss tax and illicit
flows, which is among themes to be deliberated during the summit.
The
OGP is a global platform for domestic reformers committed to making
their governments more open, accountable, and responsive to citizens.
Tanzania is among countries which have signed its membership to the OGP.
Hon
Zitto has great interest on tax avoidance through illicit transfers and
last year he tabled private motions which lead to the adoption of a
Parliament Resolution compelling the government to investigate a number
of individuals who have illicitly stashed billions of dollars abroad.
The
fact finding mission will see its members interact with UN Tax
Committee, OECD, EU as well as key European governments. They will visit
a number of European cities namely Geneva, Paris, Luxembourg, Brussels
and Oslo.
Issued by;
Parliamentary Office of Hon. Zitto Kabwe MP
Dar es Salaam
October 19, 2013
No comments:
Post a Comment