MOSHI wananchi wa vijiji vitano vya tambarare vilivyopo wilaya ya Moshi wanatarajia kunufaika
na mradi mkubwa wa maji ambao unatarajia kuanza kutekelezwa na serikali ya Ujerumani
kupitia shirika lake la AKO kwa gharama ya shilingi milioni mia nane na kumi (810,000,000/=) za kitanzania.
Makamu mwenyekiti wa AKO Bw. Klaus Boehme amesema asilimia sabini na tano ya
utekelezaji wa mradi huo utagharamiwa na
na serikali ya Ujerumani na asilimia 20 klabu ya rotary za Tanzania na Ujerumani
na asilimia tano wananchi wa vijiji hivyo vitano.
Bw. Boehme ameyazungumza
hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo baada kutembelea chanzo cha maji cha mananga kilichopo
katika mto Ghona ambapo ndipo mradi huo wa maji unatarajiwa kuanza, na aliendelea kusema kuwa vifaa kwaajili
ya ujenzi wa mradi huo tayari vimekamilika.
Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii Mkoani Kilimanjaro (TPP
Trust) utakao simamia utekelezaji wa mradi huo wa maji Bw. Sindibadi Mlaki amesema baada ya kukamilika mradi huo utakabidhiwa
kwa jumuia ya watumia maji wa vijiji hivyo vitano vya kata ya kilema kusini.
Akipokea mradi huo kwa niaba ya serikali katibu tawala wa wilaya
ya Moshi Bi. Remida Ibrahimu amewataka wananchi wa vijiji hivyo kuwa walinzi wa
mradi huo ili uwe endelevu kwa faida yao na vizazi vijavyo.
Vijiji vitakavyo nufaika na mradi huo ni pamoja na kilema pofu, kilema chini, kilototoni, masaera
na kijiji cha masae kyura.
No comments:
Post a Comment