Afisa
mmoja mwandamizi wa chama cha Democrat nchini Marekani, senata Harry
Reid, amesema kuwa baraza la senate litaiwekea Iran vikwazo vipya mwezi
ujao, iwapo mazungumzo yanayoendelea mjini Geneva, kuhusu mpango wake wa
nuklia hayatafualu.
Wajumbe kutoka mataifa sita yenye ushawishi
mkubwa duniani, ikiwemo Marekani, zinajaribu kuafikia mkataba wa awali
ambao utawala wa Tehran utasaini kuidhinisha kupunguza urutubishaji wa
madini ya uranium ili jamii ya kimataifa ilegeze baadhi ya vikwazo
vilivyoiwekea.Lakini baadhi ya masineta wanasema wana wasi wasi kuwa mkataba huo hautotosha kudhibiti mpango huo wa Iran.
Baada ya siku mbili za mazungumzo mjini Geneva, mjumbe mmoja wa Iran alisema kuwa maswala muhimu yangali kujadiliwa wakati mjumbe mwingine akisema kuna umuhimu wa kuondoa kile anachosema ni vizingiti vinavyotatiza mazungumzo hayo.
No comments:
Post a Comment