John Kessy (aliyevaa Tshirt nyekundu) akiwa na rafiki yake kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon.
John Kessy (Tshirt nyekundu) akifurahi baada ya kumaliza kilometa 42 na kukabidhiwa medali
Tshirt zinazouzwa na John Kessy kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto
wanaishi katika mazingira magumu.
John Kessy akiwakabidhi wanafunzi pesa ili waweze kulipa ada.
Wanafunzi wakifurahia baada ya kukabidhiwa pesa ya kulipa pesa ya kulipa ada na John Kessy.
Wanafunzi wakilipa ada kwa mwalimu wao.
John Kessy akiwa amesimama na baadhi ya watoto aliofanikiwa kuwalipia ada.
MOSHI kwa takribani miaka kumi na
mbili imezoeleka kuwa kila mwezi wa february au March katika uwanja wa ushirika
mkoa wa Kilimanjaro hufanyika mashindano ya kukimbia maarufu kama “Kilimanjaro
Marathon” na watu kutoka mataifa
mbalimbali duniani hushiriki katika mbio hizo. Mbio hizo ambazo zimegawanyika
katika makundi manne ambayo ni “FULL MARATHON” ambayo ni kilimeta 42, “HALF
MARATHON” ambayo ni kilometa 21, “RUN FOR FUN” ambayo ni kilometa 5, na “SPECIAL
MARATHON” ambayo ni kwa ajili ya walemavu wa viungo ambao hutumia “wheel chair” hukimbia kilometa 10.
Kwa kutumia fursa ya mbio za “Kilimanajaro
marathon” John Kessy ambaye ni mkazi wa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro amae ni
afisa maeendeleo ya jamii hususani katika kundi la vijana na watoto, pia ni
mwanasosholojia wa kijamii katika nyanja ya elimu, afya na haki za watoto na
vijana. John amekuwa akishiriki katika
mbio za “Kilimanjaro marathon” kwa zaidi ya mara sita ambapo alikua akikimbia “HALF
MARATHON” lakini mwaka huu aliamua kukimbia “FULL MARATHON” kwa lengo la
kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia kuwalipia ada na sare watoto wa shule za
msingi zilizopo katika manispaa ya Moshi wanaoishi katika mazingira magumu.
Kauli mbio ya mpango huu wa kusaidia
elimu ya watoto ilikuwa ni "RUN FOR A PURPOSE” yaani “KIMBIA KWA MALENGO” na “ONE KILOMETER
ONE KID IN SCHOOL” yaani “KILA KILOMETA MOJA ATAKAYOKIMBIA JOHN KESSY MTOTO
MMOJA ATAKUA AMEWEZESHWA KUENDELEA NA SHULE”
Lengo la John Kessy lilikuwa kukusanya zaidi ya fedha za kitanzania
milioni tatu na laki sita (3,600,000/=) kutoka kwa wasamaria mbalimbali ili
kufanikisha lengo hilo ambapo kila mtoto angetumia kiasi cha shilingi elfu
dhemanini na tano (85,000/=) kwa kulipa
ada na sare za shule.
Hadi kufikia leo tarehe 26 March 2014
John Kessy amefanikiwa kukusanya jumla
ya fedha ya kitanzania milioni mbili na laki tano. Na tayari baadhi ya watoto
wameanza kulipiwa ada pamoja na kupata sare mpya za shule watoto zaidi ya
ishirini na saba (27). Na John anasisitiza kuwa bado nafasi ipo wazi kwa yeyote
atakaeguswa na lengo hili la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira
magumu.
Pia kuna Tshirts nzuri ambazo upande
wa mbele zimeandikwa “ONE KILOMETER ONE KID IN SCHOOL” na upande wa nyuma
zimeandikwa “RUN FOR A PURPOSE” ambazo
kama utanunua Tshirt hizo utakuwa
umesaidia lengo hili la kuwasaidi hawa watoto. Na ikumbukwe kwamba watoto hawa wanaosaidiwa ni watoto
wanaishi katika mazingira magumu.
Wasiliana na John Kessy kupitia namba
hizi hapa:-
+255 (0)782 090 699 au +255 (0)754 090 699.
No comments:
Post a Comment