Dar es Salaam. Wakati Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likipandisha bei ya umeme kwa zaidi ya asilimia 40, limetakiwa kulipa zaidi ya Sh844.8 bilioni, kwa kampuni zilizoifungulia kesi mbili tofauti kwa kukiuka mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya IPTL.
Baada ya shirika hilo kushindwa kesi hiyo, sasa
limepoteza pia haki ya kumiliki mitambo ya IPTL ikiwa ni mwaka mmoja tu
kabla ya muda wa kuikodisha ufikie kikomo na mitambo hiyo iwe mali ya
Tanesco kwa asilimia 100.
Mkataba huo wa kukodisha mitambo hiyo wa miaka 20 ulioingiwa mwaka 1995, ulikuwa ufikie kikomo mwaka 2015.
Kiasi hicho cha fedha ni sawa na kiasi cha fedha ambazo kinapangwa kwa ajili ya bajeti za wizara nyeti nchini.
Wakati Tanesco ikitakiwa kulipa deni hilo la
Sh884.5 bilioni, mapato yake kwa mujibu wa bajeti ya 2012/2013, ni kati
ya Sh60 bilioni na Sh70 bilioni kwa mwezi, huku matumizi yake yakiwa
Sh11 bilioni.
Taarifa ambazo gazeti hili limezipata, zinaeleza
kuwa Tanesco ilikuwa na kesi mbili, moja iliyofunguliwa jijini Dar es
Salaam na nyingine Washington DC nchini Marekani.
Kwa upande wa kesi ya jijini Dar es Salaam, hukumu
yake ilitolewa na Jaji John Utamwa wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, Januari 17 mwaka 2014 saa 8:30 usiku.
Hukumu hiyo imeanza kuzua maswali mengi kiwa baadhi ya watu wakihoji kwa nini itolewe usiku na siyo mchana.
Hukumu nyingine ni ile iliyotolewa Februari 12
mwaka 2014 na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya
Uwekezaji cha Washington DC nchini Marekani.
Katika kesi ya jijini Dar es Salaam, mdai alikuwa
ni VIP Engineering and Marketing LMT pamoja na Independent Power
Tanzania (IPT).
Wajibu madai katika kesi hiyo walikuwa ni Pan
Africa Power Solutions T (LTD), Benki Kuu ya Tanzania ambako Tanesco
walikuwa wamefungua akaunti maalumu (ESCROW Account), Stanbic Tanzania
Ltd pamoja na UBL Bank Tanzania LTD.
Kwenye kesi ya Washington, Standard Charted Bank
(Hong Kong) Limited, iliishtaki Tanesco kwa kukiuka mkataba wa kushindwa
kuwalipa ushuru wa Dola za Marekani 2.5 milioni kila mwezi.
No comments:
Post a Comment