Katika jambo ambalo limevuta hisia za wanafunzi wengi na
walimu wa Chuo cha Mwenge ni Tukio lililotokea leo Majira ya Jioni hii katika
Chuo cha Mwenge kilichopo Moshi.
Kwa Mujibu wa mzazi wa watoto wanaotuhumiwa kubakwa alieleza tukio zima
kuwa siku ya ijumaa majira ya Jioni Binti yake (Jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 15 na ni
mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Maki Sekondari iliyoko
Olele huko Marangu Kitowo alitoweka nyumbani Huko Marangu Kitowo akiwa na mwenzake (jina la Jina linahifadhiwa) mwenye umri wa Miaka kumi
na sita na hawakuweza kuonekana mpaka jumapili jioni. Baada ya kuonekana ndipo
walipobanwa na kusema walikua Moshi mjini kwa Mwanaume ambaye alikua ni mwalimu
wao shuleni na anasoma chuo cha Mwenge.
Afisa wa Polisi anayeshughulikia Dawati la Jinsia na Watoto Afande Kasusura akiwa amemkamata Mtuhumiwa mmoja aitwaye Majaliwa nje ya chuo cha Mwenge.
Baada ya maelezo ya watoto ha Jeshi la polisi kwa
kushirikiana na Wazazi wa watoto hao ndipo walipofika katika chuo hicho na kuweza kuwatia mbaroni
wanafunzi hao mdugu Sebastian Mashauza Mwenyeji wa Kigoma na ni mwanafunzi wa
Mwaka wa kwanza na Mwenzake alitambulika
kwa jina moja la Majaliwa Mwenyeji wa Kigoma na ni mwanafunzi wa mwaka wa
kwanza katika chuo hicho.
Mtuhumiwa akioneshwa watoto alioshiriki kuwabaka waliopo ndani ya Gari kabla ya kwenda kuonesha mwenzake alipo.
Mmoja wa waathiriwa akizungumza na muandishi wetu alisema Anamtambua
Sebastian Mashauza kama mwalimu wake alikuja shuleni kwao akawa anawafundisha
somo la Kiswahili, Baada ya mwezi mmoja aliondoka wakawa wanawasiliana kwa njia
ya simu na siku ya ijumaa ndio mwalimu huyo akamtumia shilingi elfu kumi kwa
njia ya M Pesa ili aje mjini na akamwambia aje na mwenzake ndipo alipomuomba Rafiki
yake Kresta amsindikize na walipofika ulipofika usiku Mwalimu huyo akamshawishi
walale ndipo amwalimu huyo alipomwambia Kresta alale na Rafiki yake aitwae
Majaliwa. Mwanafunzi huyo alizidi kusema
kuwa walipotaka kuondoka siku inayofuata hawakupewa nauli ndipo ikapelekea
walale tena mpaka siku ya jumapili walipopewa nauli na kuondoka kurudi
nyumbani.
Afande Kasusura akimpeleka Mtuhumiwa kuonesha mwenzake alipo.
Hata hivyo uchunguzi wa awali umebaini kuwa
Sebastian Mashauza alifundisha katika shule ya Maki sekondari anayosoma Mmoja wa wanafunzi hao na alikua kama mwalimu wa field hapo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kwa sasa
watuhumiwa wako Kituo cha Polisi cha Marangu tayari kwa kusubiri Utaratibu wa
kisheria kukamilika kabla ya kupelekwa Mahakamani.
Majaliwa akitolewa ndani ya nyumba wanayoishi na ndio nyumba iliyotumika kuwabaka watoto hao baada ya mwenzake kupatikana
Mtuhumiwa namba moja Sebastian Mashauza mwalimu aliyewarubuni wanafunzi wake akiwa chini ya ulinzi mkali.
No comments:
Post a Comment